NECTA yaijibu Green Acres.

Tanzania Daima kwa mara nyingine linajiingiza kwenye kuchapisha habari bila utafiti wa kutosha!!!
 
huyo Mkurugenzi wa Green Acres nae akili yake haiba akili, na Wahariri wa Magazeti wameonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye hilo..
 
Who to believe! Baraza la mitihani au Mkurugenzi wa shule.
Kama haya ya kwenye press release yatakuwa ni kweli kama inavyoonyesha. Huu utakuwa ni uzembe wa hali ya juu na kama sivyo, basi wahariri wanafahamu vizuri nia na madhumuni ya kuandika habari zilizopinda kwa manufaa ya wanaowafahamu wawo.

Inashangaza mambo ya msingi kabisa ya uandishi yanawekwa pembeni au kuwa overlooked. Kwani kulikuwa na gharama gani ya kuhakiki kama maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa shule ni sahihi.

Tanzania Daima linaanza kuonyesha kama liko desperate kwa 'mission' mpaka wahariri wanasahau majukumu yao ya msingi kabisa. Katika wiki moja limekuja na madudu ambayo habari zake bado ni sensitive nchini.
 
Tanzania Daima kwa mara nyingine linajiingiza kwenye kuchapisha habari bila utafiti wa kutosha!!!

kweli,km necta ni mkweli,basi waandishi ni makanjanja. Ilihitaji dk kama kumi tu na resources kidogo,kufanya research ya baadhi ya mambo.mfano kujua km mwanafunzi Y amewekewa matokeo au laa!,ni swala la pale news room kuconfirm kwenye mtandao. Pia mwandishi alipashwa kuwasikiliza na upande wa pili,yaani necta wao wana data gani! Kweli hapa wameingizwa cha kike!
 
Bujugo analeta siasa ili shule ionekane imeonewa ila hiyo summary inatosha kujua hapo hakuna excuse. A winner sets commitment and a looser goes for shortcuts.
 

Mimi sipendi na wala sitawalaumu waandishi wa HABARI hata siku moja na nitakuwa wa mwisho pekee yangu kufanya hivyo. HUYU MKURUGENZI WA GREEN ACRES alidanganywa na CLOUDS RADIO kuhidhalilisha NECTA eti kwasababu NECTA WAMEWALALAMIKIWA WAO KWA KUMPROMOTE YULE DOGO MWAKA JANA ALIEANDIKA BONGO FLAVA KAMA SHUJAA. Sasa mwaka huu vijana wamemchukulia yule kijana kama role model wao then kuchora kwingi. Sasa waandishi wameripoti vile vielelezo alivyovitoa yule mkurugenzi ambayo pia ni journalism. Clouds ni radio ya MABWEGEEEEEEE
 
Eti naye mkurugenzi wa Green Acres ana PhD, toka darasa la saba, haya anayofanya kwa kishwa chake ni SAIZI YAKE MNO...
 
Hapo kuna walakini juu ya habari hii, kwa ushahidi wa baraza ni wazi kabisa watahiniwa hao matokeo yao ni sahihi. Swali la msingi ilikuwaje aje aitishe press conference ili hali hana data za kutosha???
 
Chezea kwingine sio NECTA. NECTA wako makini sana jamani. Ebu soma barua yao na vielelezo utapata jibu. Mimi natamani sana hata vyuo vyetu vya elimu ya juu viwe na umakini katika kazi hasa linapokuja suala la mitihani kama NECTA.


Safi sana NECTA! Hadi karatasi ya mahudhurio imeletwa, duh! Ingekua kwingine, sijui hii karatasi ingekuwa wapi sasa!
 
Mkuu una uhuru wa kutowalaumu waandishi wa habari lakini kwenye hii habari lazima tu wabebe lawama kwa sababu mazingira ya habari yenyewe katika misingi ya uandishi wa habari walitakiwa kwanza kuihakiki.

Katika hili swala, kuna pande tatu katika tukio ( mkurugenzi, baraza la mitihani na waandishi). Makosa au uongo wa mkurugenzi hauwezi kuwaondoa katika kashfa ambayo inasababishwa na uzembe au makusudi kutuletea habari. Lazima nao pia wapate kipande chao cha lawama kama waleta habari.
 
Mkuu kwa mtu yeyote makini alishagundua kuna walakini kwa huyo mkurugenzi, maana kama kuna tatizo ameliona kwenye shule yake kwanini asikwenda NECTA kupata uhakika wa kile anachokisema, unaposhidwa kupeleka malalamiko yako sehemu husika ni ujinga, ninapata mashaka na huyo mkurugenzi wa hiyo shule au ndio mambo ya biashara hayo
 

Pouwa mkuu, pamoja sana!
 
Acheni siasa/porojo za vijiweni
kwenye mambo ya kitaalam
kama elimu, tuachieni
wataalam tujadili na
kurekebisha dosari
zilizosababisha kufeli kwa form
four 2013! Nashangaa
MALUMPENI wamekurupuka
from no where kila mtu na
hoja zake dhaifu za vijiweni
mmesomea wapi ualimu au
mnadhani walimu
wanachaguliwa kwa kufumba
macho na kunyosha mikono
juu!!
 
Sijakuelewa mkuu hizo stori za vijiweni au siasa ni zipi kwenye hii thread wakati sisi tunajadili NECTA ilivyokosoa habari za haya magazeti tajwa
 
Mkurugenzi amechemka mazima,ni aibu sana pamoja na wahariri wauza magazeti wasiofuata taaluma yao,mitandao iko wazi kabisa wangeangalia dak 5 tu wange ignore press conference ya huyo Mkurugezi wa Shule hiyo!alitaka ku justify matokeo yafutwe waanze upya?imekula kwake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…