NECTA yaijibu Green Acres.


mkuu ungekuwa unajua waandishi walio wengi bongo ni ushuzii usingepoteza muda wako hata kutoa maoni yako yaani ukishawapa hela tu wataandika tofauti na mawazo ya wengine..

Ref: kesi ya eddy macha na gazeti la mwananchi
 
NECTA tunawashukuru sana, wapi twaweza wafikishia maoni yetu?kazi yenu tumeikubali na nataman nchi hii kila taasisi ya serikali iwe kama ninyi!umakini wa hali ya juu,kuzingatia maadili na kujibu hoja kwa hoja na uthibitisho!big up NECTA...elimu haitaki siasa,mnastahili hongera kutoka kwa kila Mtanzania mwenye kuipenda hii nchi.
 

Haupo sahihi sana, jiulize kwanini kwenye hiyo barua Tanzania Daima hawajalaumiwa aliyelaumiwa ni mkuu na mkurugenzi wa shule. Ukipata jibu utaelewa magazeti kazi yao ni kutuhabarisha yote.

Tungejuaje kama mkurugenzi wa shule ni muongo kama hii habari ingechimbiwa shimo???
 
Tanzania Daima kwa mara nyingine linajiingiza kwenye kuchapisha habari bila utafiti wa kutosha!!!

Rejea mleta mada amesema: "Kufuatia habari zilizoandikwa kwenye magazeti zikinukuu tuhuma za makosa ya NECTA katika mitihani ya wanafunzi wa shule hiyo. Baraza la mitihani limetoa jibu rasmi". Sasa wapi Tanzania Daima imetajwa?? Naheshimu sana sana mada zako Ze Marcopolo, lakini sasa naona unataka kutulisha maneno yako, hatudanganyiki!!!
 

Shikamoo mama yangu mdogo. Samahani kwa kuraise eye brows zako, lakini mpendwa mama mdogo naomba usome taarifa ya NECTA sentensi ya kwanza. Narudia tena mpendwa mama mdogo samahani kwa kukukwaza, sio lengo hata kidogo kumkwaza mama yangu mdogo.
 
Hii shule imezoea kununua mitiani, so Mwaka Jana hawakufanikiwa Ikala kwao, anatafuta HURUMA watu wasiwatoe watoto wako,

Nilishasema Hii shule ya Masista DOOO na Wavaa MILEGEZO tu,

Hapa Tz shule nyingi zimezoea kuiba mitiani na sasa wamebanwa ndo wanaanza kulia lia, hawana lolote matokeo yamewaumbua.
 
Shikamoo mama yangu mdogo. Samahani kwa kuraise eye brows zako, lakini mpendwa mama mdogo naomba usome taarifa ya NECTA sentensi ya kwanza. Narudia tena mpendwa mama mdogo samahani kwa kukukwaza, sio lengo hata kidogo kumkwaza mama yangu mdogo.

Marahaba mdogo wangu!!! Ndiyo haswa umeenda nilikotaka useme, pale pametajwa magazeti la Tanzania Daima na Mtanzania, kwa nini umeshupalia Tanzania Daima??? Why? Why? Why?
 
Marahaba mdogo wangu!!! Ndiyo haswa umeenda nilikotaka useme, pale pametajwa gazeti la Tanzania Daima na Mtanzania, kwa nini umeshupalia Tanzania Daima??? Why? Why? Why?

Mkuu wangu mama mdogo, nakupa heshima yako kwa mara nyingine na kukuomba tena msamaha kwa kukukwaza. Katika post yangu ya awali kuhusu Tanzania Daima kuna neno TENA. Neno hili ndio key word (neno funguo). Gazeti hilo la chadema liko kwenye mahojiano na polisi juu ya habari ya uchochezi inayohusu vurugu za Geita. Kabla hata hayo hayajaisha linakuja tena na "technical error" nyingine.
Naheshimu sana michango ya vyombo vya habari katika kutoa ajira na habari kwa umma, lakini weredi ni jambo la msingi katika fani hii ya uandishi kama jinsi ilivyo kwa fani nyingine.

Hata hivyo najisikia vibaya kukukwaza mama yangu mdogo na nitajitahidi nisiwe nakukwaza tena. usichoke kunikumbusha mwanao ninapokukosea, ndio u-mama wenyewe huo. nakutakia weekend nyororo. Tuendelee kuwa pamoja...
 


Ze Marco Polo, sasa umeeleweka, kwa mchango wako wa kina changanya na hii kutoelewka kulikokuwa kumetokea, nakupa hii poster ya ujumbe wa leo ikupoze!!. Tuko pamoja!!

 
NECTA ni wa ukweli bana haya magazeti na radio mbao yafungiwe maana yanapotosha umma
 
Tanzania Daima ni gazeti lakufungia vitumbua tu
 
Bujugo mabae ndio mkurugenzi wa Green acres ni mwanasiasa [ Diwani ] na pia yuko kibiashsra zaidi kuliko kitaaluma!! Alifikiria kwa kufanya alivyofanya atakuwa anaepusha lawama za kufeli kwa shule yake.
 

Nzowa mbona mapovu tena vipi bana, tunajua walimu wanapatikana kutoka kwenye gredi gani ya watahiniwa ndio, kwani hatujui?

Kama mko wataalamu mlikuwa wapi kabla matokeo ya watoto wetu hayajawa hivi? Unataka tuwaachie tena nyinyi waalimu mtafute suluhisho?

LUMPENI mwenyewe
 
Chama kinachomiliki gazeti la Tanzania daima ni bora wakaligeuza kuwa gazeti la udaku litawafaa sana
 
Hivi mnakumbuka matokeo ya mtoto wa Raisi?na ile four yake?kama NECTA waliweza kutoa matokeo ya mtoto wa mkuu wa nchi akiwa amepata division IV hivi kuna mtu anaweza kuhoji credibility ya hawa jamaa kweli? Nawaunga mkono hawa jamaa,kwa kweli hawachakachuliki wala hawalei upuuzi! Big up NECTA, this is what we want for Tanzania to develop!
 
Binafsi siwezi kuwapongeza NECTA moja kwa moja wala kumnyooshea kidole Mkurugenzi wa GREEN ACRES pia.
Ni juzi juzi tu tulishuhudia NECTA wakikosea utoaji wa matokeo ya somo la "Elimu ya Kiislamu", hivyo hata wao sio kuwa wapo makini kiasi cha kutoweza kukosea la hasha.
Pia kwa wale wenzangu mnaovinyoosha vidole vyenu kuyaelekea magazeti tajwa nadhani mtakuwa mnakosea kwa kiasi fulani. Radio, televisheni, magazeti n.k vyote ni vyombo vya habari. Kilichofanywa na magazeti haya ni kujaribu kuichokonoa NECTA ibainishe kupitia taarifa ya Bw. Julian, hivyo huwezi kuyatia hatiani magazeti hayo kwani wao hawakuwa chanzo kikuu cha Habari. Kwa kulitambua hilo ndio maqna hata NECTA imenyoosha kidole chake kukanusha taarifa iliyoandikwa(iliyotamkwa na Bw. Julian).
 

Mkuu hata kama NECTA imeshawahi kukosea lakini mie sidhani kama ni busara kuamua kutunga madai ya uongo na uzushi kabisa . Mnyine mnyongeni lakii haki yake mpeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…