NECTA yatangaza matokeo ya Darasa la Saba 2019. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 3.78

Shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ndiyo shule bora kitaifa na wanafunzi wake watano wameingia kumi bora.
 
Hayo matokeo yapo wapi
 
Mfumo WA elimu nchini Tz kwa sasa nafikiri umevurugwa sana, Kwa sababu naona hata watoto wanaohitimu kidato cha sita reasoning capacity yao iko chini sana, huwezi kuamini
 
Sasa hao necta walikuwa na maana gani kutangaza matokea wakati matokeo hayo hawajayaupload?. Yaani dunia ya sasa utangaze kitu ambacho unajua kabisa uhitaji wake ni kiubwa kisha data unaupload baada ya masaa 6 mbele? Au hawana mb?
 
Link zote zilizowekwa hapa hazifunguki sijui kwa nini!
 
Siyo kitu kigeni kwa hao watu sijui huko maofisini shughuli kubwa ni ipi.
Sasa hao necta walikuwa na maana gani kutangaza matokea wakati matokeo hayo hawajayaupload?. Yaani dunia ya sasa utangaze kitu ambacho unajua kabisa uhitaji wake ni kiubwa kisha data unaupload baada ya masaa 6 mbele? Au hawana mb?
 
Tulizoea ufaulu wa watoto wawili au watano kwenye shule kwenda sekondari le mnatuambia asilimia hizo??? Je wasiojua kusoma na kuandika ni wangapi na mtawajuaje ikiwa tumeambiwa mpaka F. 5 wapo wasiojua kusoma na kuandika? Sawa hiyo? haaaaata.
Ha ha! Mlizoea!! Ndo mabadiriko hayo!!
Itakuwa matokeo yanaongezeka kutokana na uzazi pia!! Watu wa kale si wa sasa sahivi tupo wengi hukumu ipo kwenye ajira... Waache wafauru wawezavyo form two watachujwa Tena na form 4 kila mmoja atapata tu njia yake kikubwa wasikosee njia daktari akawa huyo asiejua kusoma na kuandika..😎
 
Chato haipo? Huyo wa baraza la mitihani ajiandae kung'oka! Itakosekanaje Chato?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…