NECTA yatangaza Matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2018. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 4.96 kutoka mwaka 2017

NECTA yatangaza Matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2018. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 4.96 kutoka mwaka 2017

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Baraza la Mitihani NECTA limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (darasa la saba) ambapo matokeo yanaonyesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 4.96% tofaiti na ufaulu wa 2017 ambao ulikuwa asilimia 72.76%

Dk. Charles Msonde amesema katika tathmini ya awali kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 4.9% ikilinganishwa na 2017, amesema pia kiwango cha ufaulu wa somo la Kiingereza uko chini sana tofauti na masomo mengine

Baraza la Mitihani nchini limewafutia matokeo watahiniwa 357, waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani iliyofanyika mwaka huu 2018

"Baraza limezuia kutoka matokeo ya watahiniwa zaidi 100 kutokana na kuugua kipindi cha mtihani na kuwapa fursa ya kufanya mtihani huo mwaka 2019" Dk. Charles Msonde

Soma pia matokeo mengine kuanzia 2008
Jumla ya watahiniwa 733,103 kati ya 943,318 wamefaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ambapo wasichana ni 382,830 sawa na 77.12% na wavulana ni 350,273 sawa na 78.38%

Takwimu zinaonyesha ufaulu katika masomo ya Kiingereza, Maarifa ya jamii, Hisabati na Sayansi umepanda kwa asilimia kati ya 4.03 na 11.92 ikilinganishwa na mwaka uliopita

Wakati huo huo, ufaulu katika somo la Kiswahili umeshuka kwa asilimia 1.44

1.jpg

2.jpg

3.jpg

4.jpg

5.jpg


Kuona matokeo hayo | Fungua link zifuatazo

http://41.59.85.99/psle/psle.htm

https://www.necta.go.tz/results/2018/psle/psle.htm
 
Back
Top Bottom