NECTA yatangaza Matokeo ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2017. Ufaulu waongezeka kwa 7.22%

NECTA yatangaza Matokeo ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2017. Ufaulu waongezeka kwa 7.22%

majiko8

Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
45
Reaction score
70
Matokeo ya Kidato cha Nne (CSEE) na maarifa (QT) 2O17 Yametangazwa na Baraza la Mtihani la Taifa NECTA.

Soma Pia Matokeo ya miaka mingine kuanzia 2008
KUONA MATOKEO

LINK 1: BOFYA HAPA

LINK 2: BOFYA HAPA

TOP.JPG


1A43C569-C588-4B29-A335-6DA4D5AABFFC.jpeg


36417A42-9E25-4F49-85AB-E460B2DE4E14.jpeg

656A9264-F12F-4545-8166-0C7A01309F1B.jpeg


==========

Akitangaza matokeo leo jijini Dar es Salaam, Katibu mkuu wa baraza la mitihani Dr Charles Msonde amesema;

Katika mtihani huo kulikuwa na watahiniwa 385, 767; wasichana wakiwa ni 198,036 sawa na 51.34% huku wavulana ni 187,731 sawa na 48.66%.

Katika mtihani huo watahiniwa wa shule walikuwa 323,332 na wa kujitegemea 62,435
Watahiniwa wa shule 317,777 sawa na 98.28% ndiyo walifanikiwa kufanya hiyo mitahani.
Wahiniwa wa kujitegemea 57,173 sawa 91.57% ndio waliofanikiwa kufanya mitihani. Mtihani wa maarifa 13,775 sawa 84.62% ndio waliofanikiwa kufanya mitihani.

Dr Msnde ameongeza kuwa, watahiniwa 287,713 sawa na 77.09% wamefaulu mitihani yao ya kidato cha nne kwa mwaka 2017 huku wasichana wakiwa ni 143,728 sawa 75.21% na wavulana ni 143,975 sawa 79.06%.

Tathimini inaonyesha ufaulu wa watahiniwa wa shule mwaka 2017 umongezeka kwa 7.22% huku ufaulu wa watahiniwa wa kujitegemea mwaka 2017 ukiongezeka kwa 6.22% na ufaulu wa watahiniwa wa mtihani wa maarifa mwaka 2017 umongezeka kwa 9.63%

Watahiniwa 10 waliofanya vizuri na shule wanazotoka ni kama ifuatavyo;

1.Felison Mdee -Marian boys
2.Elizabeth Mango -Marian girls
3.Anna Benjamin Mshana - Marian girls
4.Emanuel Lameck Makoye -Ilboru
5.Lukelo Thadeo Luoga-Ilboru
6.Fuadi Padic -Feza Boys
7.Godfrey Mwakatage -Uwata
8.Baraka Mohammed -Angels
9.Lilian Moses Katabaro -Marian girls
10Everlyn Moses Mlowe -St. Fransis Mbeya

Dr Msonde amemalizia kwa kubainisha kuwa ufaulu wa jumla kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017 umeongezeka kwa 7.7%.
 
Wangeweka mfumo wa majina hii ya kuweka namba kwenye matokeo siipendi
privacy ya mtu ni muhimu,pili majina yana mfanano mkubwa unawezan kuta jina moja wanalo watu zaidi ya wawili,so ni vyema kutumia namba.....tatu kuzuia wambea wambea wanaopenda kufuatilia mambo yasiowahusu,unataka kuona mtoto wa mwenzio kapata nini ili umcheke..
 
Wayatoe tuu maana watoto wanapresha hatariii
 
privacy ya mtu ni muhimu,pili majina yana mfanano mkubwa unawezan kuta jina moja wanalo watu zaidi ya wawili,so ni vyema kutumia namba.....tatu kuzuia wambea wambea wanaopenda kufuatilia mambo yasiowahusu,unataka kuona mtoto wa mwenzio kapata nini ili umcheke..
Inatupa taabu saana kupata matokeo ya ndugu zetu walio mbali
Privacy iwe kwa watu wazima kuanzia A Level na chuo O level na
Primary wayaanike tu.
 
Baraza la Mitihani linatarajia kutangaza matokeo ya mtihani wa taita kidato cha nne muda mfupi ujao
20180130_085602.png
 
mods hizi threads ziunganishwe, fanyeni kazi yenu vizuri... issue moja threads 10 why
 
Inatupa taabu saana kupata matokeo ya ndugu zetu walio mbali
Privacy iwe kwa watu wazima kuanzia A Level na chuo O level na
Primary wayaanike tu.
Kuna chuo kikuu kimoja hapa Tz hakina cha haya mambo ya praivesi, hata kama umedisco utakutwa umetundikwa notisi bodi
 
Back
Top Bottom