taffu69
JF-Expert Member
- Feb 26, 2007
- 2,094
- 540
Mkuu usihofu NECTA ya sasa imeweka kila kitu wazi sio kama zamani, unaweza kupata fomu ya ku-appeal kwenye tovuti ya NECTA (The National Examinations Council of Tanzania) pakua jaza kwa usahihi, lipia na kisha itume NECTA kwa huduma. Maelekezo yote ya malipo yapo kwenye fomu hiyo.
Hii ni NECTA ya uwazi na Ukweli ya kwanza kutokea Tanzania.
Usifikiri kila Mtanzania ana access na hiyo mitandao mkuu, wengine tumetumia vibatari kujisomea na mpaka sasa bado vinatumika, hizo fomu za kupakua kwenye website ya NECTA ataweza kweli kuzipata achilia mbali kulipia hiyo gharama? Transcript yenyewe kuipata ni kwa mbinde sembuse kufuatilia rufaa ya matokeo ya mtihani.
Tuwe wakweli, kwa wengine mazingira bado ni magmu mno kupata haki inayotakiwa.