KLABU ya Yanga leo hii imeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Macron wenye thamani ya Sh. Bilioni 2 kwa ajili ya utengenezaji na uuzaji wa jezi za klabu hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga, Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba mkataba utakuwa na ongezeko kutokana na makubaliano waliyofikia.
Mwakilishi wa kampuni ya Macron Tanzania Bw. Suleyman Kareem, amesema wamevutiwa na Yanga kwa sababu ni klabu kubwa nchini hivyo itakuwa vizuri kufanya kazi na klabu hiyo.