NEEMA KUU: Bwawa la Nyerere kuzalisha umeme wenye thamani sawa na 50% ya makusanyo ya TRA nchi nzima, (Trillion 12 kwa mwaka)

Kama wamefunga hii mitambo ya gesi ambayo uzalishaji wake una gharama ya juu kulipo mitambo ya hydro basi ile faida ya umeme wa maji bila kuchelewa ishushwe kwa watumiaji. Tupunguziwe bei ya umeme ili maisha yawe nafuu kwa matumizi ya nyumbani na viwanda vizalishe kwa umeme wa bei nafuu. Wawekezaji wa viwanda wataweza pia kuvutiwa na umeme wa bei nafuu. Tunajua mabeberu hawataki uwepo umeme wa bei nafuu kwenye nchi zetu ili tusiweze kupata maendeleo tuendelee kua ombaomba na soko kwa bidhaa zao.
 
Kabisa, hii ni vita ya kiuchumi, wanaogopa bei ya umeme ikishuka, viwanda vitazalisha kwa gharama ndogo na bidhaa zetu zitashindana na zao za toka nje, hii inahatarisha ajira za watu wao huko CHINA! Tuache kufungulia mabwawa na kuumwaga umeme chini, bei ishuke ili umeme utumika wote bila kubakia!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…