Kabla ya yote turudi darasani kidogo, maana sitaki tuanze kuulizana maswali obvious , mara sijui source ni ipi, nk. haya twende kazi.
Unit moja ya umeme hapa Tanganyika inauzwa kwa wastani wa shs. 600/=. Unit moja ya umeme ni kitu wanaita Kilowatthour (KWh). Kilowatthour ni nini hasa? Kilo inamaanisha ‘Maelfu’ (thousands , 000), Watt ni neno linalowakilisha kiwango cha nguvu (power), in this case ni nguvu ya umeme. Sasa hour ni lisaa (dakika 60).
Kwa mantiki hiyo, Unit moja ya umeme (1KWh), ni kipimo cha kiasi cha umeme ambacho kama utautumia kufanya kazi inayohitaji ‘power’ (nguvu) ya watts 1000 , basi unit hiyo itaisha baada ya lisaa limoja (dakika 60).
Haya sasa, tuliza akili halafu twende taretibu. Bwawa la Nyerere linatajwa kuweza kuzalisha Megawatt 2100. Hii inamaanisha nini?
Mega ni neno linalomaanisha millions (000,000), hivyo kwa tafsiri rahisi kabisa, bwawa hili linauwezo wa kuzalisha nguvu (power) ya umeme ya Watts ‘MILLION 2100’ , tukitaka kuiweka kati Kilowatts, tunagawanya hiyo namba kwa ‘1000’ , ambapo tunapata kwamba hilo bwawa linazalisha umeme wenye nguvu ya KILOWatts MILLION 2.1.
Hadi hapo tupo pamoja naamini, maana wewe unaesoma hapa naamini unaakili walau za kuemdea chooni, hivyo lazima hadi hapo umenielewa. Sasa basi , tubadilishe hicho kiwango kuwa ‘Killowatt hour’ (KWh) ambayo ndio unit moja ya umeme sasa.
Mashine za kufua umeme huo wa 2.1 million Kilowatts, zikizalisha umeme kwa muda lisaa limoja, maana yake tumezalisha Unit za umeme zipatazo Million 2.1 , yaani 2.1 million Kwh.
Unit moja ya umeme hapa Tanganyika ni 600/=; sasa kwa unit milioni 2.1, unapata milioni 1,260 ; ambayo ni bilioni 1.26 kwa lisaa. Hivyo basi kwa masaa 24 (siku 1), mitambo inazalisha umeme wenye thamani ya shillingi bilioni 30.24; kwa mwezi ni mara 30 ya hiyo, ambayo tunapata wastani wa Trillion 1 kwa mwezi.
Sasa kwa miezi 12 tunafanya mara 12, hivyo tunapata Trillion 12 kwa mwaka, ambayo ni 50% ya makusanyo yote ya TRA kwa mwaka mzima.
Sasa cha ajabu, huo umeme utauzwa nje, na bado watoto kule kondoa wataendelea kukalia vumbi darasani kwa ukosefu wa fedha za kununulia madawati, huku kesi za ICSD dhidi ya Tanesco wanazojishtaki wenyewe zikiendelea kupamba moto.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo September 20, 2023 amefungua Kongamano la Tano na Maonesho ya Nishati Tanzania na amesema kwamba Serikali imedhamiria kuwa Mzalishaji mkubwa wa nishati na kuwa na umeme wa kutosha utakaopatikana kwa urahisi na nafuu na ziada itauzwa nje ya Nchi...
Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko ameshuhudia uwashwaji wa mtambo namba tisa katika bwawa la kuzalisha umeme la Julis Nyerere JNHPP ambao umeanza kusambaza umeme megawat 235 katika gridi ya Taifa. Akishuhudia uwashwaji wa Mtambo huo wa kuzalisha umeme Dkt biteko amesema...
Kama wamefunga hii mitambo ya gesi ambayo uzalishaji wake una gharama ya juu kulipo mitambo ya hydro basi ile faida ya umeme wa maji bila kuchelewa ishushwe kwa watumiaji. Tupunguziwe bei ya umeme ili maisha yawe nafuu kwa matumizi ya nyumbani na viwanda vizalishe kwa umeme wa bei nafuu. Wawekezaji wa viwanda wataweza pia kuvutiwa na umeme wa bei nafuu. Tunajua mabeberu hawataki uwepo umeme wa bei nafuu kwenye nchi zetu ili tusiweze kupata maendeleo tuendelee kua ombaomba na soko kwa bidhaa zao.
Kama hii mitambo ya gesi ambayo uzalishaji wake una gharama ya juu kulipo mitambo ya hydro basi ile faida ya umeme wa maji bila kuchelewa ishushwe kwa watumiaji. Tupunguziwe bei ya umeme ili maisha yawe nafuu kwa matumizi ya nyumbani na viwanda vizalishe kwa umeme wa bei nafuu. Wawekezaji wa viwanda wataweza pia kuvutiwa na umeme wa bei nafuu. Tunajua mabeberu hawataki uwepo umeme wa bei nafuu kwenye nchi zetu ili tusiweze kupata maendeleo tuendelee kua ombaomba na soko kwa bidhaa zao.
Kabisa, hii ni vita ya kiuchumi, wanaogopa bei ya umeme ikishuka, viwanda vitazalisha kwa gharama ndogo na bidhaa zetu zitashindana na zao za toka nje, hii inahatarisha ajira za watu wao huko CHINA! Tuache kufungulia mabwawa na kuumwaga umeme chini, bei ishuke ili umeme utumika wote bila kubakia!
Bilionea wa kihindi Gautam Adani ameshitakiwa kwa utapeli na rushwa katika mahakama ya New York. Yeye na wenzake wanatuhumia kuahidi rushwa za mamiliono ya dola kwa maafisa wa serikali ili kupewa mikataba na tenda kimagumashi ikiwemo ya umeme wa solar. Itakumbukwa kuwa moja ya makampuni ya...
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura), imetangaza bei mpya elekezi kwa watumiaji wote wa umeme kisiwani humo ambapo zitaaza rasmi Januari 20, mwaka huu. Kwa mujibu wa Zura, ilipokea maombi ya kubadilisha bei za umeme kutoka Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kutokana na...
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema Mkoa wa Dar es Salaam ni wa kipekee katika ukusanyaji wa mapato nchini. Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda alisema hayo Dar es Salaam juzi usiku wakati wa hafla ya kuwapa tuzo walipa kodi bora wa mikoa ya kikodi ya Dar es Salaam kwa mwaka 2023/2024...
Mikoa ya kaskazini imekuwa na umeme tangu zamani. Kwa mfano Kilimanjaro kila kijiji kimeunganishwa na gridi ya Taifa. Kama rais Samia anatafuta kitu cha kuwafanyia watu wa mikoa ya kaskazini basi afanye haya: 1. Barabara za lami 2. Reli ya mpya (SGR) 3. Mipango miji 4. Viwanda Kusema ataleta...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.