NEEMA KUU: Bwawa la Nyerere kuzalisha umeme wenye thamani sawa na 50% ya makusanyo ya TRA nchi nzima, (Trillion 12 kwa mwaka)

NEEMA KUU: Bwawa la Nyerere kuzalisha umeme wenye thamani sawa na 50% ya makusanyo ya TRA nchi nzima, (Trillion 12 kwa mwaka)

Haya ni maono ya waasisi wetu,ambao ndiyo CCM wenyewe,Taifa hili bila CCM tutakwama kwasababu vingine havina mwelekeo wenye maslahi kwa Watanzania
 
kama hutaki kuulizwa maswali basi ni afadhari sana kama ungekaa na mada yako bila kushirikisha jamii
 
Kabla ya yote turudi darasani kidogo, maana sitaki tuanze kuulizana maswali obvious , mara sijui source ni ipi, nk. haya twende kazi.

Unit moja ya umeme hapa Tanganyika inauzwa kwa wastani wa shs. 600/=. Unit moja ya umeme ni kitu wanaita Kilowatthour (KWh). Kilowatthour ni nini hasa? Kilo inamaanisha ‘Maelfu’ (thousands , 000), Watt ni neno linalowakilisha kiwango cha nguvu (power), in this case ni nguvu ya umeme. Sasa hour ni lisaa (dakika 60).

Kwa mantiki hiyo, Unit moja ya umeme (1KWh), ni kipimo cha kiasi cha umeme ambacho kama utautumia kufanya kazi inayohitaji ‘power’ (nguvu) ya watts 1000 , basi unit hiyo itaisha baada ya lisaa limoja (dakika 60).

Haya sasa, tuliza akili halafu twende taretibu. Bwawa la Nyerere linatajwa kuweza kuzalisha Megawatt 2100. Hii inamaanisha nini?

Mega ni neno linalomaanisha millions (000,000), hivyo kwa tafsiri rahisi kabisa, bwawa hili linauwezo wa kuzalisha nguvu (power) ya umeme ya Watts ‘MILLION 2100’ , tukitaka kuiweka kati Kilowatts, tunagawanya hiyo namba kwa ‘1000’ , ambapo tunapata kwamba hilo bwawa linazalisha umeme wenye nguvu ya KILOWatts MILLION 2.1.

Hadi hapo tupo pamoja naamini, maana wewe unaesoma hapa naamini unaakili walau za kuemdea chooni, hivyo lazima hadi hapo umenielewa. Sasa basi , tubadilishe hicho kiwango kuwa ‘Killowatt hour’ (KWh) ambayo ndio unit moja ya umeme sasa.

Mashine za kufua umeme huo wa 2.1 million Kilowatts, zikizalisha umeme kwa muda lisaa limoja, maana yake tumezalisha Unit za umeme zipatazo Million 2.1 , yaani 2.1 million Kwh.

Unit moja ya umeme hapa Tanganyika ni 600/=; sasa kwa unit milioni 2.1, unapata milioni 1,260 ; ambayo ni bilioni 1.26 kwa lisaa. Hivyo basi kwa masaa 24 (siku 1), mitambo inazalisha umeme wenye thamani ya shillingi bilioni 30.24; kwa mwezi ni mara 30 ya hiyo, ambayo tunapata wastani wa Trillion 1 kwa mwezi.

Sasa kwa miezi 12 tunafanya mara 12, hivyo tunapata Trillion 12 kwa mwaka, ambayo ni 50% ya makusanyo yote ya TRA kwa mwaka mzima.

Sasa cha ajabu, huo umeme utauzwa nje, na bado watoto kule kondoa wataendelea kukalia vumbi darasani kwa ukosefu wa fedha za kununulia madawati, huku kesi za ICSD dhidi ya Tanesco wanazojishtaki wenyewe zikiendelea kupamba moto.

Bishana na data (Hoja), usibishane na mimi.








=========================

Tunataka umeme sio porojo. Tumekua tunalishwa maneno utafikiri tutashiba.
 
Tunataka umeme sio porojo. Tumekua tunalishwa maneno utafikiri tutashiba.
Unamwambia nani sasa, mimi ndio Tanesco? Mimi nimeleta hoja yangu kama mwananchi mfuatiliaji, jadili hoja yangu..
 
 
1CE38A93-9D9B-4F5A-84FA-393C6CB2CB26.jpeg
 

Bwawa la Nyerere litapandisha sana GDP kwa karibu asilimia 25. Tujiandae kupewa mikopo kwa lazima yenye riba hadi asilimia 50 kwa mwaka..
 
Back
Top Bottom