Neema Swai: Sifungi ndoa na Mrema

Naipendatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
5,096
Reaction score
8,234
"Siolewi na Mzee Mrema, hizi habari zinazozushwa na picha yangu kusambaza mtandao kuwa naolewa naye ni uongo na uzushi. Picha inayosambaa ni yangu niliipost kwenye page yangu watu wakaichukua na kuiunganisha na ya Mzee Mrema na kuisambaza mtandaoni"

"Simjui Mzee Mrema na sijawahi kukutana naye. Nilikuwa nimelala asubuhi naamka nakuta missed call nyingi. Kwenye wathsaap nikatumiwa Screen shot kuwa naolewa na Mrema" Neema Swai, Mwanafunzi wa CBE anayedaiwa kuolewa na Mwenyekiti wa TLP, Lyatonga Mrema.


Source: Clouds TV
 

Kama hii ni habari kubwa, kuna katiba mpya kweli hapa hata 2040?
 

Na ikitokea offer ya Mwarabu wa kuchovya au mzungu utaikataa offer hiyo? Au wewe ni wakipekee duniani? 🤣🤣
 
Nausemea huo mpunga wa "masponsa" kwa akina "Navalny" wetu......

Unadhani hata kuna u Navalny au sponsor basi?

Si ujiulize kwa dhati yako tu:

"Hivi inawezekana je kwa aliyekuwa mwenyekiti wa bunge la katiba na akachukua posho, leo hajui kama watanzania wanataka katiba mpya?"

Kweli? Na wewe unaona ni sawa? Akipigiwa kelele huyo, ili mseme kuna Navalny au sponsor?

Kwa kutuona je vile?
 
Itakuwa Mrema alienda kuongea na Mzee Swai, babaake na huyo binti wakayamaliza kiutu uzima

Mzee labda keshalamba mahali. Haiwezi kuzuka taarifa ghafla hivi bila sababu.

 
Umeongea nae kaburini?!!!

Mjomba una kipaji cha kuongea na wafu.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…