Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Mfano, yale Maghorofa ya pale "faya". Naona ni aina fulani ya uchafu usiostahili kuwepo pale miaka hii aisee.
Watu wanaleta emotions tu ila hawana fact hata moja yaan ushindwe kuboresha mandhari ya mji na kuongeza tija ya majengo sababu eti kuna wapangaji hili jambo uliliona wapi duniani uchumi uliobora ni ule unaoendeshwa kwa mising ya uchumi wa soko.
Kama kipato chako ni cha kukaa bunju usitake kulazimisha kukaa upanga.
Watu wanataka kuzeekea kwenye nyumba za NHC kisa kodi za dezo afu haohao ndo kutwa kwenye mabar na mitandaoni kuwaponda wenzao waliojenga chanika mbagala kibamba n.k kuwa wanakaa maporini.
MCHECHU yupo mbele ya muda watu wenye upeo mdogo hawawez kumuelewa lakin kwa wanaojua historia ya NHC alipoitoa na alipoifikisha wote watamuunga mkono kwenye harakati za kuliboresha shirika kwa kuliongezea project zenye tija na kupendezesha mji pia maana nyumba zote za NHC pale city center ni kama maghofu tu kwa kuanzia na zile za upanga.
 
Nehemia ni aina ya watendaji wapendao sifa za kijinga na mshirika wa mafisadi na ndiyo maana JPM alimla kichwa.

Vilevile, huyo ni mmoja wa waliorejeshwa na Samia ili kumkomoa marehemu JPM 😄
Very stupid and childish arguments....
Mtu aliekufa na kuoza anakomolewaje!?
Yaan kuna watu hawaamini km Magufuli alishakufa😂😂
 
Inawezekana vipi, mkataba wangu na wa jirani yangu tuliopanga apartments za aina moja utofautiane kwenye kiasi cha kodi tunacholipa!? Huoni huu utakuwa ndio mwanzo wa rushwa!? Kwamba mpangaji anaweza toa rushwa ili apewe nafuu kwenye kodi!? Hii haikubaliki.
Haijarishi mnakaa apartment zenye kufanana, lakini kila apartment anatazamwa kama kitu specific na kila mteja anachukulia kama individual, hivyo mkataba wa mpangaji mmoja haulazimiki kuwa sawa na wa mpangaji mwingine. Kwa kuwa malipo hayo hufanyika kimkataba, maana yake NHC wanayafanya hayo ndani ya taratibu zao za kisheria. Kama kuna rushwa inayofanyika basi Rushwa hiyo haiwezi kufichwa ndani ya mkataba, bali huwa nje ya mkataba.

Yote kwa yote, mteja asiyeridhika na huo mtindo wa mikataba ya NHC, busara ni kuachana na nyumba za NHC ili kutafuta mahali pengine. Zipo taasisi nyingi za umma zenye kutoa huduma hafifu (kama TTCL, TRC) huwezi kuona watu wakilazimisha kuzikumbatia kwa kuwa kuna taasisi mbadala zenye kutoa huduma kama zao katika ubora, huko ndiko kitakimbiliwa. Wakimbieni hao NHC kama inawezekana!!
 
Huo ni udalali na ni wizi wa mchana kweupe. Na ni wazi unajaribu kuyafanya maisha ya watu magumu zaidi. Ni kama uingie supermarket kisha ukute bidhaa hazijawekwa bei. Yaani bei anakutajia yule mhudumu. Waliobandika bei unaona walikuwa wajinga!?
 
Huyo mtu wa hali ya chini anaishi upanga, almuntzar ?
Watu wachache weusi wameshika zile nyumba wanawakodishia wahindi kwa bei ghali huku wenyewe wakiilipa NHC hela kiduchu.
Majina ya wapangaji ni wamatumbi ila wanaoishi ni wahindi
Haya mambo yapo pia kota za urafiki sheklango
Hayo ni matatizo yao NHC kushindwa kufanya proper management, kwanza walitakiwa waweke limit ya mtu kupanga kwenye hizo nyumba isizidi miaka mitano ili kutoa fursa kwa wengine wenye uhitaji. Sasa mtu hadi anapata wajukuu bado ni mpangaji wa NHC.......vinginevyo wangekuwa wana review mikataba baada ya miaka mitano ili anaetaka kuendelea alipe kodi kubwa zaidi kutokana na soko lilivyo. Hii itaondoa uwezekano wa watu ambao tayari wana uwezo wa kujenga au kununua nyumba zao kuendelea kuhodhi nyumba za NHC.
 
Back
Top Bottom