Nawasalimu kwa jina pendwa la JMT..Kazi iendelee.
Ni jambo la kushangaza eti Nelson Mandela aliyekuwa Kiongozi mpigania Uhuru wa Afrika Kusini kuitwa Baba wa Amani Afrika..
Inawezekanaje mtu aliyewasaliti watu wake kisa kutolewa jela na kusaini makubaliano ya kuhalalisha uporaji wa Ardhi ya Weusi uliofanywa na Boers eti anaitwa Shujaa na kusherekewa?
Huyu bwana alihalalisha Eneo la asilimia 80% la Ardhi ya Afrika Kusini kumilikiwa na Boers ambao ni chini ya 20% ya Watu huko Africa Kusini..
Yet mtu kama huyu eti Afrika inamuona ni shujaa,huyu ni shujaa wa Wazungu ndio wanapaswa kumfurahia.
Uhuru ni Ardhi sio bendera sasa huna Ardhi wewe si ni kijakazi tuu.? Yaani wenzake wamwage damu kwa ajili ya kupigania Ardhi ila yeye akaishia kuwapa hiyo ardhi ilimradi tuu ametolewa jela na kupewa madaraka ya kisiasa..
Ona watu wake wanavyoteseka na wamefikia mahala kuua ndugu zao wa damu kwa kupumbazwa na Wazungu wahamiaji..
Mandela hafai kabisa kuwa mfano kwa vizazi vyetu, kiongozi pekee wa kupigwa mfano hapa Afrika angalau ni Mwl.J.K Nyerere.