Nelson Mandela alihalalisha uporwaji wa Ardhi ya Afrika Kusini kwa Boers halafu anaitwa Baba wa Afrika. Afrika tumerogwa na nani?

Nelson Mandela alihalalisha uporwaji wa Ardhi ya Afrika Kusini kwa Boers halafu anaitwa Baba wa Afrika. Afrika tumerogwa na nani?

Uko sahihi kabisa! sijui jamaa walimfanya nn hadi kusaliti watu wake kiasi hiki! aliwasaliti pakubwa sana aisee
Jamaa alisahau wema wote aliotendewa na waafrica wenzie katika kupigania uhuru wao alishindwa hata kuudhuria msiba wa Nyerere
 
Nawasalimu kwa jina pendwa la JMT..Kazi iendelee.

Ni jambo la kushangaza eti Nelson Mandela aliyekuwa Kiongozi mpigania Uhuru wa Afrika Kusini kuitwa Baba wa Amani Afrika..

Inawezekanaje mtu aliyewasaliti watu wake kisa kutolewa jela na kusaini makubaliano ya kuhalalisha uporaji wa Ardhi ya Weusi uliofanywa na Boers eti anaitwa Shujaa na kusherekewa?

Huyu bwana alihalalisha Eneo la asilimia 80% la Ardhi ya Afrika Kusini kumilikiwa na Boers ambao ni chini ya 20% ya Watu huko Africa Kusini..

Yet mtu kama huyu eti Afrika inamuona ni shujaa,huyu ni shujaa wa Wazungu ndio wanapaswa kumfurahia.

Uhuru ni Ardhi sio bendera sasa huna Ardhi wewe si ni kijakazi tuu.? Yaani wenzake wamwage damu kwa ajili ya kupigania Ardhi ila yeye akaishia kuwapa hiyo ardhi ilimradi tuu ametolewa jela na kupewa madaraka ya kisiasa..

Ona watu wake wanavyoteseka na wamefikia mahala kuua ndugu zao wa damu kwa kupumbazwa na Wazungu wahamiaji..

Mandela hafai kabisa kuwa mfano kwa vizazi vyetu, kiongozi pekee wa kupigwa mfano hapa Afrika angalau ni Mwl.J.K Nyerere.
Unamzungumzia Nyerere huyu mchonga meno aliyemlaghai rais karume wa Zanzibar nchi yao kutawaliwa tena ni koloni la Tanganyika?

Mchonga meno aliyelipeleka jeshi la Zanzibar na kuuawa kwa wanajeshi wa zanzibar kadhaa katika vita ya kumuondoa Idiamini wa Uganda Madarakani, huku akipeleka askari wachche kutoka upande wake Tanganyika?
Unajua migogoro iliyopo leo Zanzibar na Tanganyika yeye ndio chanzo? Zanzibar ni nchi huru lakini rais wao anachaguliwa ni Watanganyika walioketi dodoma? unadhani alistahili kuitwa baba wa taifa?
 
Wakati mwingine busara na hekima vitawale, wa South wanajeuri ya shibe ndugu yangu, Zimbabwe ile pale wamechukua kila kitu yako wapi sasa?

na hiyo shibe wameipata kutokana na mzungu ila wanashindwa kufahamu hilo
 
Back
Top Bottom