Nelson OKWA: Sivunji mkataba wangu bila mil. 800/=

Nelson OKWA: Sivunji mkataba wangu bila mil. 800/=

Kisa tu eti alionekana kukinukisha kwenye mechi 2 alizocheza dhidi ya Yanga alipokuwa Rivers United! Wazee wa kukurupuka wakampa mkataba!! Huku wakimpamba kwa kila aina ya mapambio.

Ngoja tuone mwisho wa hili sekeseke! Milioni 800 usawa huu, si mchezo.
Kwani vipi kuhusu Bigirimana????yeye alikinukisha wapi mpaka mkamsajili?
Kambole je???????maana haya yote ni magarasa,list ni ndefu kuna kina kalengo,yipke,moringa,kindoki n.k
Lielewe soka ndio ulizungumzie ,katika suala la usajili wa wachezaji kuna mengi,sio kila anayeflop hajui na kupeleka lawama kwa wanaosajili

Kuna mchezaji kuzoea mazingira,kuna suala la tabia,kuna suala la mifumo vyote hivi vinaaffect viwango vya wachezaji hasa newcomers......
 
Mikataba ya Simba inaandikwa na watu wanaojielewa ndio maana migogoro kati ya Simba na wachezaji ni adimu sana
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kwani vipi kuhusu Bigirimana????yeye alikinukisha wapi mpaka mkamsajili?
Kambole je???????maana haya yote ni magarasa,list ni ndefu kuna kina kalengo,yipke,moringa,kindoki n.k
Lielewe soka ndio ulizungumzie ,katika suala la usajili wa wachezaji kuna mengi,sio kila anayeflop hajui na kupeleka lawama kwa wanaosajili

Kuna mchezaji kuzoea mazingira,kuna suala la tabia,kuna suala la mifumo vyote hivi vinaaffect viwango vya wachezaji hasa newcomers......
Mimi sijamlaumu mtu. Halafu hao wachezaji uliowataja hapo juu, umesikia yeyote kati yao amewahi kuigomea klabu kuondoka mpaka alipwe kiasi kikubwa cha pesa? Jibi litakuwa ni hapana!

Maana yake nini; walisajiliwa kwa kiwango kidogo cha fedha! Na haikushangaza kuona hata mashabiki tuliwalalamikia hao wachezaji, pamoja na viongozi walio wasajili.
 
Kisa tu eti alionekana kukinukisha kwenye mechi 2 alizocheza dhidi ya Yanga alipokuwa Rivers United! Wazee wa kukurupuka wakampa mkataba!! Huku wakimpamba kwa kila aina ya mapambio.

Ngoja tuone mwisho wa hili sekeseke! Milioni 800 usawa huu, si mchezo.
Ila mi nahisi inawezekana kuna kitu hakipo sawa... inawezekana ni mchezaji mzuri sema amekosa confidence uwanjani... siamini kama ni mbovu hivo
 
Utailamu Kamati ya Usajili, lakini mimi naungana na Magori kuwa mtu anayepaswa kusajili wachezaji na viongozi wa klabu na sio kocha. Kocha sio mpenzi wala mwanachama wa klabu, ukimpa madaraka ya kusajili mchezaji kwa mkataba wa miaka mitatu wakati yeye hana uhakika wa kudumu kwa hata miezi sita, unafanya makosa. Kocha ndiye aliyependekeza wasajiliwe Okwa na Ouatara, halafu yeye akapata ofa nene sehemu nyingine akawaacha Simba!
Sitamsahau Kocha Zolani. Alikuja kuiharibu Simba.
Watani wakapata fulsa wakatuchapa 2 : 1
Watara alikuwa anamsindikiza tu Mayele.
 
Habari za kuaminika kutoka kwenye vyanzo vyenu kama kawaida. Tanzania ndiyo inayoongoza kwa habari za uzushi kipindi cha usajilj.
 
Acha kupotosha wewe hiyo pesa hata gharama ya usajili wake yeye haifiki Milioni 800, mkataba wa mwaka mmoja hauwezi kuwa na thamani ya kuvunjwa kwa kiasi hicho.
Kuvunja mkataba kuna kulipa fidia mkuu.. hata ivyo haowezi kufika iyo hela labda ni mbinu za kutaka kuwapiga hata machinga ukiulizia bidhaa ya elfu 15 atakwambua elfu 50 alijua hata ukimsusha mtaishia kwenye elfu 30 au 25
 
Sitamsahau Kocha Zolani. Alikuja kuiharibu Simba.
Watani wakapata fulsa wakatuchapa 2 : 1
Watara alikuwa anamsindikiza tu Mayele.
Hata mkiwa na yule mfaransa milipigwa 1-0 kwenye semi final ya fa msimu jana
 
Suala la muda tu ataachwa..hata Dubai haendi...yeye na Akpan hawajaenda Dubai kwa sababu za kiuhamiaji(sidhani kama ni kweli nadhani hapa hawa mwendo wameumaliza)
 
Kuvunja mkataba kuna kulipa fidia mkuu.. hata ivyo haowezi kufika iyo hela labda ni mbinu za kutaka kuwapiga hata machinga ukiulizia bidhaa ya elfu 15 atakwambua elfu 50 alijua hata ukimsusha mtaishia kwenye elfu 30 au 25
Mkataba wao umeuona huyo Mnaija sio mbongo.
 
Huyo kijana hata kukimbia hawezi. Kukaba hawezi
Kupiga pasi sahihi hawezi
Kamati ya Usajiri ya Simba ina dhana bado kuwa kila mchezaji mfupi ni Miquissone.
Aliyeharibu simba ni yule kocha zoran alisema anamtaka outarra na okwa halafu akaja na shemegi yake mzungu halafu akakimbia akaacha team ndio maana team kubwa ulaya suala la kusajili ni la raisi na sio kocha maana kocha mda wowote anaondoka anaacha mizigo kama hyo
 
Back
Top Bottom