Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Mkuu samahani kwa kauli hii, ningependa kujua elimu yako ni kiwango gani?
Kama umefikia elimu ya shahada ya kwanza kuna kitu hakiko sawa ktk mfumo wako wa kujifunza ukiwa shuleni na vyuoni.

The wisdom in philosophy
From the Latin sapientia, it relates to intelligence, in the opinion, common sense, prudence, knowledge, science, philosophy. Wisdom is commonly used to describe the character of that which is reasonable, or to exercise moderation in desires.
Source: What is Wisdom ? Philosophical Definition

Ukisoma hapo kwenye nini maana ya wisdom(hekima) utaona inahusiana na vitu vingi ikiwemo na knowledge, science na phylosophy.

Je elimu ya chuo kikuu lengo lake sio kukupatia knowledge?
Je kazi ya chuo kikuu sio kukupa mbinu za kisayansi na kutambua asili ya vitu kisayansi?
Au kutafuta majibu ya vitu mbalimbali au changamoto mabalimbali zinazo ikabili jamii au dunia kwa njia za kisayansi kupitia hizo tafiti (research) unazo sema?

Go back to the college mkuu wangu.
 
hiyo picha ya mwenge ni uchuro tu hapo na ndiyo maana inazalisha wazee wa jalalani.
Huelewi hapo maana yake Ni the book that has strong light that shines.

Ukiweka litabu kubwa mwanga mdogo maana yake Ni hopeless the book that has no light and that does not shine

Wasomi wa UDSM wanna shine Sana maraisi wengi wameputia UDSM was kwetu na was nchi zingine

Nembo la chadema halina mwenge ndio maana ha li shine
 
Naomba nitofautiane na wewe; lengo la msingi la chuo kikuu ni kupata KNOWLEDGE not WISDOM! Ni kupata MAARIFA sio HEKIMA! Hakuna mahali popote darasani uliwahi kukaa ili ufundishwe HEKIMA; tunaingia darasani kupata MAARIFA. Huwezi kuniambia wote ambao hawajafikia elimu ya chuo kikuu au ambao hawajasoma (darasani) kabisa hawana HEKIMA!

"Where is the wisdom we have lost in knowledge? Where is the knowledge we have lost in information?" —T.S. Eliot. Knowledge is gathered from learning and education, while most say that wisdom is gathered from day-to-day experiences and is a state of being wise. Knowledge is merely having clarity of facts and truths, while wisdom is the practical ability to make consistently good decisions in life.
 
umeandika ugoro mtupu
 
'Hekima ni uhuru', sijui hata maana yake ni nini.
Tasfiri yake MTU aliyeelimika huwa na hekima hekima maana yake ukiwa na maarifa utakuwa huru.MTU aliyesoma apaswi kutembea gizani bali nuruni,ukiwa na hekima upo nuruni
 
Wivu tu kwa ambao hawakubahatika kusoma UDSM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tasfiri yake MTU aliyeelimika huwa na hekima hekima maana yake ukiwa na maarifa utakuwa huru.MTU aliyesoma apaswi kutembea gizani bali nuruni,ukiwa na hekima upo nuruni
HEKIMA inachangiwa na vitu vingi sio elimu ya darasani peke yake; na wala hakuna shule au chuo chochote kinachofundisha HEKIMA. Jukumu la msingi la chuo kikuu chochote ni kutoa MAARIFA so slogan ya UDSM iendane na jukumu lake la msingi - MAARIFA. HEKIMA ni matokeo ya vitu vingi katika maisha na sio elimu ya darasani peke yake!
 
Wale ambao hamjakutana na mtaara wa hekima piteni kimya kimya m like hapa.
Mengine tutajua mbele kwa mbele.
 
Una hoja ya msingi sana mkuu.Wahusika waitafakari.
 
Hata hiyo ya tumaini ni same kwa muktadha wako maana msalaba ndio mkubwa kuliko vyote hivyo ni kisiasa za kidini au?!
 
Kuhusu alama ya mwenge wa uhuru (Torch of Freedom) au (Uhuru Torch)
Nyerere alikuwa anawaza mbali sana.
Yule mtu alikuwa mwanafunzi wa falsafa ktk maisha yake.

Ukiachana na maneno yake kuhusu sababu za kuwasha mwenge siku ya Uhuru na Mzee Nyirenda kwenda kupandisha juu ya kile cha mlima Kilimanjaro, kulikuwa na ujumbe mwingine Nyerere anautuma kwa lugha ya picha ya mafumbo.

Naweza kusema ule mwenge ni ujumbe katika lugha hiyo hapo juu ambayo niite ni metaphorical kwa kimombo.

Kwa kufupisha ule mwemge unatoa mwanga, mwanga katika fikra. It is a symbol of enlightenment.
Ni kwamba Nyerere alikuwa anaturudisha kifikra ktk zama za Enlightenment (Age of Enlightenment).
Enlightenment maana yake ni UFUNUO wa fikra.

Enlightenment (Ufunuo wa fikra) ni muunganiko wa dhana mbalimbali zilizo jikita katika masuala ya uhuru wa kuhoji au kudadisi (reasoning) na ushuhuda wa hisia kama vyanzo vya msingi vya maarifa na dhana za juu kabisa kama za Uhuru, maendeleo, uvumilivu, undugu, serikali za kikatiba na kutenganisha serikali(dola) na dini.

Kizungu tunasema:
"The Enlightenment included a range of ideas centered on the sovereignty of reason and the evidence of the senses as the primary sources of knowledge and advanced ideals such as liberty, progress, toleration, fraternity, constitutional government and separation of church and state." source : Age of Enlightenment - Wikipedia

Utaona hayo yote juu ni maaana au tafsiri ya University wakati huo zina anzishwa kule dola ya kirumi. Sisi tumeiga tu.

Natamani sasa wabobezi kama akina Prof Mukandala waje wanirekebishe na kuichambua vizuri hii hoja yangu.

Maana mimi ni mchanga sana kielimu na ni mtu wa sayansi hii ya hisabati, na tehama sio haya mavitu makubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…