Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Naomba ufafanue iko sawa kivipi.
Logo ya chuo kikuu haiwezi kuwa Kama ya shule ya msingi au shule ya upili ya kuanza kuongelea education tu au Maarifa tu. Chuo kikuu lazima ujumbe wa logo yake uwe na maana pana. Na ndivyo ulivyo ujumbe wa chuo kikuu. Kumbuka hiki ni chuo cha kihistoria nchini mwetu. Cha kwanza kutoa elimu kwa wazalendo bila ubaguzi.
 
Salary Slip ana hasira na CCM, Sasa anajisahau na kuleta hadi kwenye maswala yasiyohitaji CCM wala UKAWA.
 
“He who learns must suffer. And even in our sleep pain that cannot forget falls drop by drop upon the heart, and in our despair, against our will, there comes wisdom to us by the awful grace of God”
(Aeschylus)
 
Ahaha Wengi mtaani wanasemaga ni freemason mara blah blah kibao..

Skia ni ivi...


Wakati wana waisraeli walivyo kua Safarini kuelekea nchi ya Ahadi mnakumbuka Kuna kisanga kilitokea pale Musa akaambiwa achukue nyoka amtundike mtini iwe kama ishara ya Uponyaji na Kila aliye Mtizama Kwa imani ya Kupona Alipona na Kuishi


HES. 21:8-32

Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi
Hiyo alama ya nyoka kwenye nembo ya Tumaini ina maanisha nini?
 
Kwani shida nn apo uhuru ama nn
 
Hekima inasomewa darasani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi unaelewa nini unapoambiwa tunatarajia wewe msomi uwe na busara na ustaarabu kuliko mtu mwenye elimu ndogo au ambae hajasoma?

Kwani inategemewa msomi afanye maamuzi kwa hekima kubwa kuliko mbumbumbu?

Endelea kusoma commet zangu zilizo fuata uone nilivyo fafanua zaidi tafsiri ya hekima(widom) na maarifa (knowledge) kwa kuangalia tafsiri ya hekima kama zilivyo elezewa na wana falsafa wakubwa.
 
Mafundisho unayopata chuo kikuu huleta au huongeza maarifa(knowledge), maarifa huongeza hekima.
Hekima inaenda sambamba na uhuru wa fikra.
 
Kwa muktadha wa maelezo yako unaonekana uliwahi kwenda shule, lakini haijakusaidia. Badala ya kuangalia hoja na hitaji la mtoa mada wewe unakimbilia kwenye mrengo wa siasa na kudhalilisha watu. Yeye alitoa dukuduku lake lililohitaji maelezo au majibu. Kama huna jibu ya nini kum-attack mtoa hoja? Una matatizo gani? Kama unafahamu hata mambo ya GPA unashindwaje kudhibiti mihemko yako? Nini tatizo lako? Wewe katika maisha sharti ujue kuna kutofautiana. Watu wotw hawawezi kuwa CCM wale CUF kwa wakati mmoja. Huoni wengine walikuwa Chadema na sasa ni CCM na kinyume chake? Unatakiwa ukue kiakili
 
Ama kweli Hekima ni Uhuru. Ukikosa hekima kama aliyeandika mada hii akili yako haiwezi kuwa huru.

Hekima ni byproduct ya knowledge. Ninamashaka na elimu uliyonayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni hizo, mnataka tuweke alama ya msalaba na nyoka? Km ulaya? Wakati tuna waislamu?

Hayo ni yetu wao wazungu ndo watuige siyo sisi tuwaige tuuu!
Tatizo mnaongea sana kwanza tumejitahidi

Siasa ni kila kitu Duniani. Huwezi jitenga na siasa daima dumu.
 
Kwa maoni yangu mwenge hauna shida hapo.Mwenge ndio unaowakilisha dhana ya hekima maana unaangaza. Hapo hakuna kitu chochote kibaya.Mwenge hauna shida yoyote,kuweka alama ya kitabu haina maana yoyote endapo bado tutakuwa kwenye hali hii hii ya mfumo huu wa elimu.

Suala hapo ni kubadili sera na mifumo elimu ili iendane na wakati lakin mwenge hauna shida.Maneno hayo ni mazuri zaidi ya slogani zote unazozijua duniani hii chini ya mbingu.Kama hekima ingewekwa mbele kama wenzao walivyofanya awamu za nyuma mambo yangekuwa vizuri.Lakini awamu ya 5 wao kwao hekima ni upuuzi ndio maana kila siku wanaonekana kama midori wasio hata na haya wala soni.
Inasikitisha



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…