Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Logo ya chuo kikuu haiwezi kuwa Kama ya shule ya msingi au shule ya upili ya kuanza kuongelea education tu au Maarifa tu. Chuo kikuu lazima ujumbe wa logo yake uwe na maana pana. Na ndivyo ulivyo ujumbe wa chuo kikuu. Kumbuka hiki ni chuo cha kihistoria nchini mwetu. Cha kwanza kutoa elimu kwa wazalendo bila ubaguzi.Naomba ufafanue iko sawa kivipi.
Shetani, kuna kitabu cha dini hakina neno shetani?Hiyo alama ya nyoka kwenye nembo ya Tumaini ina maanisha nini?
Hekima kila MTU anayo kinachotafutwa ni maarifa ya kutumia hekima,ni lazima usome ili uendane na Ulimwengu wa kimaarifa na utambuzi/ethical issues.
PumbavuMawazo mgando, ndio maana makao makuu ya pale ufipa yanazidi kutitia.
Hayo ni matokeo ya elimu uliyopata!Kuna baadhi ya mambo tunahoji hayana logic yoyote.......anyway sisi WaTz ujuaji umezidi sana wakati hatujui
Hiyo alama ya nyoka kwenye nembo ya Tumaini ina maanisha nini?
Kwani shida nn apo uhuru ama nnHabari wakuu,
Binafsi napenda kushauri viongozi wa Chuo hiki kuitazama upya nembo ya chuo kama kweli nembo hiyo inastahili kubaki kama ilivyo au ifanyiwe marekebisho madogo ili iwezeke kusadifu zaidi maswala ya academic kuliko ilivo sasa ambapo,kwa mtazamo wangu,inasadifu zaidi siasa za miaka ya nyuma.
Naposema imekaa kisiasa zaidi simanishi haibebi ujumbe wowote wa kitaaluma, bali ni kwasababu imetoa nafasi kubwa kwa maswala ya kisiasa {mchoro wa Mwenge} kwenye nembo huku mchoro wa kitabu ukipewa nafasi ndogo wakati kazi ya msingi ya chuo ni kuzalisha wataalamu.
Nachojiuliza,mchoro wa Mwenge kwenye nembo ya taasisi inayotoa taaluma inasaidifu nini? Inawezekana nembo ya chuo hiki ni ile ile tangu uhuru hivyo kwa wakati huo, labda kulikuwa na sababu ya kuweka mchoro wa mwenge katika nembo ya chuo ila sidhani kama ni sahihi kuendelea kuwa na mchoro huo kwa wakati tulionao.
Ukiacha mbali swala la mchoro huo wa mwenge,hata maneno yaliyoko katika slogan hiyo nayo sidhani kama yana uhusiano wowote na chuo hicho ambacho kazi yake kubwa ni kuzalisha wataalam(wasomi).
Maneno yaliyoko katika nembo hiyo ni haya:hekima ni uhuru.
Nembo husika ni hii:
Kwa maneno hayo ambayo bila shaka ndio kauli mbiu ya chuo,ni wazi yanaturudisha kule kule kwenye mchoro wa mwenge wa uhuru jambo linalonifanya nijiulize ilitokea tu kama coincedence au ni jambo lililokuwa limekusudiwa?
Nadhani wakati umefika nembo hii itazamwe upya na ifanyiwe marekebisho madogo ingawa jambo hili nalo linaweza kuwa na changamoto zake ingawa sitaki kuamini changamoto hizo ndio zinaweza kuwa kikwazo zaidi tu ya kukosekana dhamira ya kuifanyia mabadiliko nembo hiyo na pengine ni kwakuwa tumeridhika nayo,tumeizoea na hatuoni kasoro yoyote katika hiyo nembo.
Hembu tazameni nembo ya chuo hki kichanga lakini inayosadifu zaidi taaluma kuliko mambo mengine yote katika nembo hiyo bila kusahau uchaguzi mzuri wa maneno yaliyowekwa katika nembo husika.
Jambo hili inawezekana liko hata katika taasisi nyingine lakini haimanishi tukae kimya.
Kama wahusika mpo humu,basi tupeni ufafanuzi wa hiyo logo na hiyo kauli mbiu(moto) labda tunaweza kuelewa.
Mawazo mgando, ndio maana makao makuu ya pale ufipa yanazidi kutitia.
Hivi unaelewa nini unapoambiwa tunatarajia wewe msomi uwe na busara na ustaarabu kuliko mtu mwenye elimu ndogo au ambae hajasoma?
Mafundisho unayopata chuo kikuu huleta au huongeza maarifa(knowledge), maarifa huongeza hekima.Hekima haifundishwi popote! Kazi ya msingi ya chuo kikuu chochote ni kufundisha, tafiti, na ushauri. Nani duniani humu amewahi kufikia "Hekima ya Sulemani"? Alisomea chuo kikuu kipi kuipata hekima ile? UDSM ijikite kwenye majukumu yake ya msingi badala ya kuambatana na siasa uchwara!
Mawazo mgando, ndio maana makao makuu ya pale ufipa yanazidi kutitia.
WaTz ujuaji mwingi sana,ukiwemo wewe unayejiona msomiHayo ni matokeo ya elimu uliyopata!
Kwa muktadha wa maelezo yako unaonekana uliwahi kwenda shule, lakini haijakusaidia. Badala ya kuangalia hoja na hitaji la mtoa mada wewe unakimbilia kwenye mrengo wa siasa na kudhalilisha watu. Yeye alitoa dukuduku lake lililohitaji maelezo au majibu. Kama huna jibu ya nini kum-attack mtoa hoja? Una matatizo gani? Kama unafahamu hata mambo ya GPA unashindwaje kudhibiti mihemko yako? Nini tatizo lako? Wewe katika maisha sharti ujue kuna kutofautiana. Watu wotw hawawezi kuwa CCM wale CUF kwa wakati mmoja. Huoni wengine walikuwa Chadema na sasa ni CCM na kinyume chake? Unatakiwa ukue kiakiliKweli wazungu walileta mfumo wa vyama vingi kutugawa hasa hiki kizazi cha sasa ambacho hakina misingi ni shida, alafu wamedakwa kule Ufipa ndiyo balaa kwenye GPA za 32.
Nembo hii inashida gani jamani maneno ya uhuru, mwenge wa uhuru, maji. Nakama tukiwasikiliza hawa wapumbafu walah tutakosa hata historia yetu hatutaijua.
Na ukishindwa kujiharalisha kisiasa utajiharalisha kwa nembo ya chuo, kweli kifo cha mende kimekaribia tutasikia mengi mara nembo ya taifa ina siasa na ukabila, kesho utasikia bendera ya taifa ina siasa za CCM rangi ya kijani ibadirishwe iwekwe ya nyekundu ya ufipa.
Ni upumbafu na ulofa katika ubora wake (Ben William Mkapa hakukosea)