Nembo ya Simba imebadilishwa na nani?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Logo ya Simba imebadilishwa na kuidhinishwa kutumika.

Swali langu ni je, taratibu za kuibadili na kuitumia nembo mpya ya Simba zimefuatwa?
 
Wameichukua tu Google wakaipachika neno simba sports club...

Tazama picha kwa umakini.. logo wameichukua google kisha wakaigeuza kutoka kuangalia kushoto na kwenda kuangalia kulia.. hiyo kitu hata kwa simu yako unaweza kufanya kwa app za picha.. kisha wakaweka neno simba sports club na rangi nyekundu tu.. badala ya blue ile ya picha halisi google.
 
Attachments

  • 20200820_104525.jpg
    28.2 KB · Views: 2
Kua uyaone!! Sasa ww taratibu zinakuhusu nn!!

Sent from my MAR-LX1M using JamiiForums mobile app
Walioibuni nembo ile ya Simba walikuwa watu na wazee wenye akili zao, na walihusisha watu wengi sana na pengine hata kamati za ufundi. Bila shaka unapotaka kuibadili lazima kuwepo na sababu maalumu shirikishi za kuibadili pia. Je, kanuni na taratibu za Simba zinasermaje kuhusu kubadili nembo au katiba ya club?
 
Minalia na jezi tu.jezi,,jezi,,jezi.Simba kwenye jezi wamenikata moto.
 
Je, mo mwenye 51% anayo haki ya kubadili chochote kwa mujibu wa katiba?

Utopolo mmeanza chokochoko, hebu mkae mtulie huko na mavyura yenu pale bwawani!

Kwani hata akiibadili jina ikiitwa mo fc inakuuma nini?

Hebu tuwekee ule mkataba mliosaini sijui na laliga tuone ni kipengele gani kinachowafanya kila mara mnakuwa na chokochoko na mabingwa wa nchi!
 
Taratibu gani hizo unazozijua ambazo unahisi hazijafuatwa?
Unayo katiba ya Simba SC hapo utuwekee hizo kanuni?
Kuuliza si ujinga, Kama katiba iya Simba inaruhusu sema tu hivyo kwa kutaja kifungu na Aya ya katiba yetu ya Simba
 
Simba na Yanga sio timu Kama Azam au Gwambina, hizi Ni timu za wananchi. Nembo sio kitu Cha mchezo. Mfano mtu ataweza vipi kuibadili nembo ya Taifa bila taifa kufahamu?
 
Logo ya Simba imebadilishwa na kuidhinishwa kutumika.

Swali langu ni je, taratibu za kuibadili na kuitumia nembo mpya ya Simba zimefuatwa?
Umewahi kuhoji kuhusu Manchester City kubadili Logo?
 
Simba na Yanga sio timu Kama Azam au Gwambina, hizi Ni timu za wananchi. Nembo sio kitu Cha mchezo. Mfano mtu ataweza vipi kuibadili nembo ya Taifa bila taifa kufahamu?
Unajua logo ya Simba imebadilishwa Mara ngapi?
 
Unajua logo ya Simba imebadilishwa Mara ngapi?
Sio msahafu kwamba haiwezi kubadilishwa, lakini inabadilishwaje? Ni mahitaji ya Nani? Ni wazo la Nani? Kukidhi haja gani? Nani wanasema hapo sawa hapo sio sawa?
 
Hivi nyie utopolo mbona mbawashwa?
Sie wapenzi ndio tulitaka ibadilishwe
Simba na Yanga sio timu Kama Azam au Gwambina, hizi Ni timu za wananchi. Nembo sio kitu Cha mchezo. Mfano mtu ataweza vipi kuibadili nembo ya Taifa bila taifa kufahamu?
 
Hata wao Man City bila shaka waliibadili ya kwao kwa mujibu wa katiba na kanuni za club yao. Nauliza kuhusu taratibu za Simba sio Man City
Kwani wewe ulitaka taratibu gani. Logo kubadilisha kuna mambo mengi yanaangaliwa hasa soko.
 
Ww una tabia kama za Lisu. Inawezekana una undugu na lisu au mnatoka kijiji kimoja au pengine mlisoma darasa moja mwalimu wenu mmoja.

Sent from my LG-K520 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…