Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 819
- 1,093
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imeandaa maonesho ya siku tatu kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupunguza taka yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Machi mwaka huu, katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yaliyobeba Kauli mbiu isemayo "𝑲𝒖𝒘𝒆𝒛𝒆𝒔𝒉𝒂 𝒕𝒂𝒌𝒂 𝑺𝒊𝒇𝒖𝒓𝒊 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝑺𝒆𝒌𝒕𝒂 𝒚𝒂 𝒏𝒈𝒖𝒐 𝒏𝒂 𝒎𝒊𝒕𝒊𝒏𝒅𝒐" yataambatana na maonesho mbalimbali yatakayoonesha namna ambavyo taka ni fursa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za Baraza Leo, Meneja Uzingatiaji wa Sheria (NEMC) Bi. Amina Kibola amesema Baraza limejipanga kutoa elimu iliyobeba dhana ya 𝐏𝐮𝐧𝐠𝐮𝐳𝐚, 𝐓𝐮𝐦𝐢𝐚 𝐓𝐞𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐑𝐞𝐣𝐞𝐥𝐞𝐳𝐚 kwa maendeleo endelevu ya Mazingira huku ikiambatana na shughuli mbalimbali za kimazingira.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191, kifungu cha 114 hadi 119 Baraza limepewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria, kutoa elimu kwa Umma kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa muongozo huo
Baraza linahimiza wananchi wote waliopo Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani kukaribia viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 12 jioni kupata elimu ya masuala ya taka hasa ikizingatiwaTaka ni fursa".