NEMC kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kupunguza Taka, kuanzia tarehe 28 hadi 30 Machi 2025

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imeandaa maonesho ya siku tatu kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupunguza taka yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Machi mwaka huu, katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yaliyobeba Kauli mbiu isemayo "๐‘ฒ๐’–๐’˜๐’†๐’›๐’†๐’”๐’‰๐’‚ ๐’•๐’‚๐’Œ๐’‚ ๐‘บ๐’Š๐’‡๐’–๐’“๐’Š ๐’Œ๐’˜๐’†๐’๐’š๐’† ๐‘บ๐’†๐’Œ๐’•๐’‚ ๐’š๐’‚ ๐’๐’ˆ๐’–๐’ ๐’๐’‚ ๐’Ž๐’Š๐’•๐’Š๐’๐’…๐’" yataambatana na maonesho mbalimbali yatakayoonesha namna ambavyo taka ni fursa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za Baraza Leo, Meneja Uzingatiaji wa Sheria (NEMC) Bi. Amina Kibola amesema Baraza limejipanga kutoa elimu iliyobeba dhana ya ๐๐ฎ๐ง๐ ๐ฎ๐ณ๐š, ๐“๐ฎ๐ฆ๐ข๐š ๐“๐ž๐ง๐š ๐ง๐š ๐‘๐ž๐ฃ๐ž๐ฅ๐ž๐ณ๐š kwa maendeleo endelevu ya Mazingira huku ikiambatana na shughuli mbalimbali za kimazingira.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191, kifungu cha 114 hadi 119 Baraza limepewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria, kutoa elimu kwa Umma kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa muongozo huo

Baraza linahimiza wananchi wote waliopo Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani kukaribia viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 12 jioni kupata elimu ya masuala ya taka hasa ikizingatiwaTaka ni fursa".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ