NEMC kuchukua hatua kali dhidi ya nyumba za ibada na sehemu za starehe zinazopiga kelele kwenye makazi ya watu

NEMC kuchukua hatua kali dhidi ya nyumba za ibada na sehemu za starehe zinazopiga kelele kwenye makazi ya watu

Ila KUNA MAKANISA YAPO KARIBU NA MAKAZI YA WATU.

Yaani unakuta kanisa lipo kati kati ya nyumba za watu, Sasa bana ikifika ijumaa hadi jumapili inabidi muhame kwanza maana siyo kwa MZIKI HUO.

======

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wametoa onyo kwa wamiliki wa sehemu za kuabudu na nyumba za starehe wanaosababisha kelele kwenye makazi ya watu na kusisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa ikiwa pamoja kufunga maeneo hayo
Misikiti itoe zile adhana na spika. Mabaa yote huku mitaani yawe na sound proof pamoja na hayo makanisa yenye fujo.
 
Misikiti ina nafuu kwakuwa wanafanya ibada kwa dakika chache sana tofauti na makanisa yanayokesha na midundo ya miziki
Unatumia nini kufikiria?? Adhana inakera sana. Maneno ya kiarabu kelele tupu alfajiri mpaka usiku.
 
Kule posta misikitini inafunga barabara ijumaa na kuswali hapo barabarani na watu hawajalalamika.
Nadhani watu wa mipango miji wanastahili lawama, ingefaa wanapopima viwanja nyumba za ibada zitengewe maeneo makubwa ili kuwepo maeneo ya kutosha kufanyia ibada hata kwa nje
 
Ila KUNA MAKANISA YAPO KARIBU NA MAKAZI YA WATU.

Yaani unakuta kanisa lipo kati kati ya nyumba za watu, Sasa bana ikifika ijumaa hadi jumapili inabidi muhame kwanza maana siyo kwa mziki huo, na hii sio mara ya kwanza kwa wao kutoa tamko kama hili

Pia soma: NEMC kufanya msako wa wanaopiga kelele nyakati za usiku kwa kiwango kilichozidi Desibeli 40

======

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wametoa onyo kwa wamiliki wa sehemu za kuabudu na nyumba za starehe wanaosababisha kelele kwenye makazi ya watu na kusisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa ikiwa pamoja kufunga maeneo hayo
washasema sana hawa.Waanze kazi si wanakuwa waongeaji tu.
 
naona adhana na kengele zina enda kuwa za sailensa...

wagosi waliomba nyundo za sailensa...
 
Wanipe kazi ya kuwafungia Sound proof Makanisani, ili kuzuia Sauti kutoka nje...!
 
Arusha Arusha Arusha,waende huko Ni balaaa Watanzania hawalali huko na ni kerooooo
 
Back
Top Bottom