super thinker
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 371
- 110
Baraza la taifa la mazingira na mamlaka husika wananchi wenu tunateseka sana na makelele ya bar zilizopo kata ya Goba, mtaa wa Kulangwa kuanzia JOY ES LAVA, DEEZ PUB, LIVE LONGUE, MUSU PARK, BAMBA BEER na kuendelea
Imekuwa sio sehemu tena ya kuishi kwa amani, na furaha ukizingatia ni eneo la makazi ya wakazi wengi sana hapa, suala limesharipotiwa serikali ya mtaa bila mafanikio
Inashangaza binadamu anakosa utu namna hii kupiga makelele usiku kucha, kwa sauti ya juu ilihali akijua ni muda wa watu kupumzika, na anajua wakazi waliomzunguka ni wengi na nyumba zina watoto wadogo, wazee, wagonjwa etc. Ni dhambi hata kwa Mungu, hakuna tofauti na kumtupia uchafu jirani
Mara nyingi kelele ni kwa namna ya disco la wazi, bendi za wazi, kelele za madj na maMC kupiga makelele muda wa usiku kwa shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye bar hzo mara nyingi mpaka asubuhi, tunalala saa ngapi na kwenda makazini saa ngapi?!?!
NEMC na Mamlaka husika tunaomba msaada kwani madhara ya kelele hizi kwa wakazi hapa ni za muda mrefu, malalamiko yameshapelekwa sehemu kadhaaa kama serikali ya mtaa bila mafanikio tulalamike kwa nani????
Ushauri: BAR HIZI ZISHURUTISHWE KUWEKWA VIDHIBITI SAUTI, PASITOKE KELELE NJE YA ENEO WANAPOPIGA KELELE KWANI WANAOTESEKA NI WENGI SANA KULIKO WANAOFAIDIKA. KINYUME NA HAPO BAR ITAKAYOKAIDI ISIMAMISHWE KUFANYA SHUGHULI MPAKA ITAKAPOTII
MFANO NINAVYOANDIKA HUU UZI MUDA HUU NI SAA 9 USIKU, KELELE HIZI BAR ZIPO JUU, WATOTO WADOGO, WAGONJWA, WAZEE HALI NI MBAYA, TUNAOMBA MSAADA KWA MANUFAA YA WAKAZI WENGI WA MTAA WA KULANGWA, KATA YA GOBA NA TAIFA KWA UJUMLA,
TUNAOMBA USHAURI PIA KWA MWENYE UZOEFU, NAMNA BORA YA KUFIKISHA MALALAMIKO HAYA YAFANYIWE KAZI KWA UHARAKA!!