Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Wapangaji wa Shirika la Nyumba zilizopo karibu na Manispaa ya Morogoro tunalalamika baa maarufu ya Ellis iliyopo karibu na Ofisi za Manispaa ya Morogoro, kuwa inapiga kupiga mziki mkubwa hadi asubuhi hali ambayo ni kero kubwa kwetu, Mamlaka husika imezungumzia suala hilo:
Kusoma hoja ya Mdau, bofya hapa ~ Baa ya Ellis (Morogoro) imerejea tabia ya kupiga kelele usiku kucha, Serikali ichunguze kinachofanyika usiku
MAJIBU YA NEMC - MOROGORO
Meneja Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mkoa wa Morogoro, Abel Sembeka amesema:
Malalamiko kuhusu hii baa sio kitu kigeni tulishachukua hatua ikiwemo kuwapa barua ya onyo na kuwapiga faini isiyopungua Shilingi Milioni 5, changamoto ilikuwa ni kelele kupita viwango vinavyotakiwa.
Baada ya kuona maalamiko hayo (kutoka JamiiForums), tumefuatilia, tumewasiliana na mmiliki wa baa na kumwambia barua inafuata.
Tutatumia Teknolojia yetu kwa ajili ya kufanya vipimo na kuangalia eneo kama linafaa kuendesha biashara hiyo kama kunakuwa na malalamiko ya mara kwa mara, anatakiwa kwenda na viwango vinavyotakiwa.
Alilipa faini hiyo, lakini inawezekana Watendaji wake wamejisahau kwa kuwa ni sehemu ya starehe.
Sisi NEMC, mteja wetu kama huyo ambaye tunakuwa tumeshampiga faini, tutafanya vipimo kwa siku ambazo yeye mwenyewe hajui, ikibainika ni kweli hatua zitachukuliwa.