Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) Dkt. Immaculate Sware Semesi ameitaka jamii yote kuzingatia maelekezo yanayotolewa na mamlaka za usimamizi na kuchukua hatua za kujilinda na hali ya hatari tarajiwa katika mazingira.
Ameyasema hayo leo tarehe 02 Februari 2025 Mkoani Dar Es Salaam wakati akiongea na Wanahabari.
Amesema, "Kama mnavyofahamu kwa miaka ya hivi karibuni, Mataifa kadhaa yamekumbwa na majanga mbalimbali yanayosababishwa na athari za shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabianchi.
Athari hizo zimetokea katika maeneo mbalimbali kuongezeka kwa joto, ukame, mafuriko na maporomoko ya ardhi. Mfano wa maeneo yaliyokumbwa na maporomoko ya ardhi katika nchi yetu ni pamoja na Katesh, Wilaya Hanang Mkoa wa Manyara, Kawetere Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya, Mamba Miamba katika Wilaya Same Mkoa wa Kilimanjaro".
Dkt. Immaculate ameongeza kwamba "Maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ni Rufiji Wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani, Wilaya za Morogoro, Malinyi, Ulanga na Kilombero katika Mkoa wa Morogoro. Maeneo yote haya yalikumbwa na mvua nyingi za juu ya wastani ambazo zilisababisha maafa kwa watu, Mifugo na mali nyingine pamoja na kuharibu miundombinu ya umma kama vile barabara, mawasiliano, umeme, maji na madaraja".
Taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), zilizotolewa Januari 23, 2025, zimetabiri uwepo wa mvua za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya mashariki mwa Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mara na Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Aidha, taarifa hiyo ya TMA iliyataja maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro, Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani.
NEMC imeyataja Madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo kuwa ni pamoja na ;
Ni wajibu wetu sote, kuhakikisha kuwa tunaweka mazingira safi na salama ili kuepusha mafuriko na mlipuko wa magonjwa ambayo yamekuwa yakirudisha nyuma jitihada zetu katika ujenzi wa Taifa.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamewatahadharisha wananchi kujiepusha kwa namna yoyote ile na vitendo vyenye kuchangia uharibifu wa mazingira kwa kuzingatia masuala kadhaa ikiwa pamoja na:
1. Kuendelea kufuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ili kuwa na tahadhari ya maeneo yenye viashiria hatarishi
2. Kuchukua tahadhari za kuepuka maeneo ya fukwe za bahari ikiwa ni pamoja na miamba ya maziwa na mito ili kujinusuru na mafuriko na athari zake.
3. Kwa wale wanaoishi kwenye maeneo ya kandokando ya milima au miinuko mikali kuchukua tahadhari ili kuepukana na athari za maporomoko ya ardhi.
4.Tunaziomba Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuatilia kwa karibu maeneo ya uchimbaji madini na vifusi ili kuhakikisha jamii husika inakuwa salama na majanga yanayoweza kujitokeza kwenye maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha udhibiti wa taka ngumu ili zisizagae na kuingia kwenye mifereji ya maji ya mvua na mifumo ya majitaka na kusababisha kuziba.
5. Abiria na wasimamizi wa vyombo vya usafiri kuwa na tahadhari wakati wa safari kwa kuzingatia kuwa maeneo ya barabara yanaweza kuwa yameathiriwa na mvua.
6. Wananchi kwenye maeneo mbalimbali kutoa taarifa kwa viongozi kwenye maeneo yao kuhusu athari zinazoweza kuwa zimejitokeza kutokana na hali hiyo.
7. Aidha, wananchi wanakumbushwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004, Kifungu Namb. 57 na kuepuka ujenzi kwenye maeneo hatarishi ikiwa ni pamoja na maeneo ya kando ya mito, mabonde, fukwe za bahari na maeneo ya ardhi oevu.
Kwa kuzingatia historia ya athari za mafuriko na maporomoko ya ardhi katika maeneo mbalimbali, ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuwa makini na kuchukua tahadhari zinazohitajika ili kupunguza madhara yanayoweza kutokea kutokana na mvua hizo.

- Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi yanayoweza kusababisha athari kubwa kwa makazi ya wananchi, uharibifu wa mashamba, upotevu wa mali na vifo.
- Athari kwa Sekta mbalimbali hasa za kilimo, mifugo, maji, maliasili na uvuvi, na hivyo kuhatarisha usalama wa chakula na ubora wa maji.
- Miundombinu ya umeme, mawasiliano, barabara, reli na maji inaweza kuathirika na kusababisha usumbufu katika upatikanaji wa huduma mbalimbali.
- Vyanzo vya maji vinaweza kuathirika na kusababisha kuziba kwa mifumo ya majitaka / mifereji na kusababisha magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na homa za matumbo.