Nendeni mkamwambie huyo mbweha hivi: 'Leo na kesho (Watu wa Mungu hawaogopi)

Nendeni mkamwambie huyo mbweha hivi: 'Leo na kesho (Watu wa Mungu hawaogopi)

Umetupeleka haraka ila usijali acha maisha acha yaenda
 
Luka 13:32
(Yesu) Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha (Herode), Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.

Hakuna watumishi wa Mungu wa ukweli wanaoogopa. Hakuna. Na hawa huwa hawatishwi na maneno ya mbweha (wanasiasa) hawa ni mbweha ambao huvaa ngozi ya kondoo. Ndani ni mbweha.

Herode alikuwa kama Rais kipindi hicho kwa nguvu alizo nazo. Yesu alimwita Mbweha. Hakuna Mtumishi ambaye atashindwa kemea dhambi kwa sababu ya mbweha hawa hawa ambao pia hutumia watumishi hao hao katika siasa zao.

Mbweha akisifiwa anafurahi. Akikosolewa anavimba na kutishia kutoa meno. Anabaki kuwa ni mbweha.
Herode hakuwa mwanasiasa, alikuwa mtawala/kiongozi mkubwa.
 
Back
Top Bottom