Mzuka wanajamvi.
Yani Papa katuangusha sana. Sasa hivi mtu unaogopa hata kubarikiwa tu na mchungaji.
Yani hata humu jamvin upande wa pili wanatudhibiti sana katika hoja pinzani kwa kutuambia Nenda kabarikiwe.
Unabaki tu umelegea na kunyong'onyea yani wanatuweza kichizi.
Neno kubarikiwa limeshuka hadhi na mantiki.
Papa kazingua sana.
Bora ugaidi na kuuza unga.
Kama utachukulia dini kama kikosi cha jeshi, kinachojiandaa kupambana vita ya silaha, au kama utaichukulia kama mtoto unayemlea hapo naweza nikasema upo sahihi na wanaokubeza pia wapo sahihi.
Ila, kama utaichukulia dini kama njia, au kimbilio baai kuna kitu mtakuwa kwa pamoja mnakosea.
Ikumbukwe, dini ni daraja la mahusiano kati ya Mungu na Wanadam, dini inapaswa kutafuta waliopotea na kuwarejesha kundini. Dini ni Daktari anayehitajiwa na Wagonjwa, sasa vipi wagonjwa hawa waambiwe wapone kwanza magonjwa yao ndipo wakamuone Daktari?
Kwanini waliopotea waambiwe watafute wenyewe njia mpaka wafike?
NI utamaduni wa kawaida kwa waumini wa dini zote kuomba baraka/dua kabla ya tukio, ni kama wanajikabidhi kwa Mungu awaongoze, sasa kuna tatizo gani kuwakabidhi (kuwabariki) mikononi mwa Mungu watu wenye tabia hizo zinazopingwa? Nadhani ni sahihi kuwabariki na kumualika Roho Mtakatifu katika maisha yao ili waweze kufunguliwa kiakili na kuiona Nuru.
Kumbariki muovu ni tofauti na kuubariki uovu, muovu anahitaji baraka ili aondokane na uovu wake.