GE2025 Neno moja tu kwa mnaoenda kupiga kura

GE2025 Neno moja tu kwa mnaoenda kupiga kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Ndugu wanagenzi, ninalo neno juu yenu!

Kuwa makini sana licha ya kwamba umehakikishiwa usalama au utalindwa, usisahau kuwa hao watu wameshachanganyikiwa ukihisiwa tu unasombwa ndani na kutoka mpaka Yesu atakaporudi. Yawezekana ulikuwa una lengo zuri tu la kwenda kupiga kura ila kwasababu tu zisizo na mbele na wala nyuma ukajikuta unaishia kutekwa, usisahau kuwa hawawezi kumtofautisha aliyejitokeza kwa lengo la kupiga na aliyejitokeza kwa lengo la kuandamana.

Kumjumlishwa ni jambo la dakika mbili tu, kuweni makini!

Hawa watu wameshapoteza ramani, wamemfunga mpinzani wao mkubwa, kwasasa kinachowachanganya ni kwamba hawajui ni nani anaekuja kuwaharibia maana adui yao mkubwa wanamshikilia wao wenyewe, so kilichobaki sasa hivi kila wanaemuona mbele wanamhisi kama mpinzani tu. usijesema hatukusema unaweza ukawa unatoka kwa lengo la kupiga kura vizuri tu ila usalama wako utafuatana na Muliro amekutazama na jicho gani.

Mimi yangu ndio hayo, tukutane pakikucha!
 
Na wamesema wana picha. Usije kuwa unafanana na mojawapo ya picha zao, kitakuramba
 
Hatari sana, nimekutana na polisi wanaomba namba hatari..!!

Nimewaambia tukutane kesho nitawapa wanasema “chondechonde usikose tutakulinda mtoto mzuri”. 😹😹😹

Kesho tutarajie kuona mengi, tunaandamana huku unapewa simu uandike namba 🤣
 
Back
Top Bottom