Neno mswahili wewe unalitafsiri vipi?

Mswahili kitaalamu ni mtu anayetokea pwani pwani huko zenji,Tanga, mtwara,Lindi,bagamoyo ila kimjinmjin mswahili Ni mtu anayekaa mazingira hatarishi(uswazi)
Ahahaha hapo ata kuna washua wanakaa mazingira hayo pia
 
Yeah Ni kweli ila utakuta asilimia kubwa wanajitenga na jamii husika ili wasiharibikiwe watoto wao
 
Mtu muongo muongo asiye muaminifu, hatimizi ahadi aliyosema kiufupi ni kwamba anaongea vitu ambavyo anajua kabisa anadanganya na wala hawazi wala kuchoka kudanganya.
 
Ni mtu fulani hivi amekaa kijanja kijanja sana, ukiwa unaongea nae mara nyingi huwa hawezi kutuliza macho sehemu moja kama katoka kuiba vile,, huyu kukupiga na kitu kizito (KUKUTAPELI) ni fasta sana.
 
KUMRADHI WANA THREAD KWA KUINGILIA MADA YENU ILA MIMI YANGU NI HAYA
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
WANANCHIIIIIII LEO NI SIKU AMBAYO
TUNAENDA KUUONESHA ULIMWENGU KWAMBA YANGA INA UKUBWA KIASI GANI.MAKOLO
WAMEJARIBU KUIKUZA MARUMO KWA KILA NAMNA ILA LEO TUTAENDA KUWAONESHA YANGA NI NANI.
EWE MWANANCHI TEMBEA KIFUA MBELE KWANI LEO NDIO TUNAENDA KUINGIA FAINALI RASMI.
LEO MADUNDUKA YATALILIA CHOONI.
 
Morng Africa

Ukilisikia neno mswahili kwako unapata maana gani yaani ukisikia mtu anaitwa mswahili ni picha gani inakujia juu ya mtu alie itwa mswahili
Kuna mswahili kabila

Kuna ushwahili umbea unafiq

Kuna kiswahili kama lugha pendwa duniani meneno yake mengi yanatokana na lugha ya kiarabu
 
Mswahili ni kabila la watu wa mwambao mambasa wapo ngazija wapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…