Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,118
- 4,238
Ukiangalia kuna chaneli kama makundi matatu hivi juu ya uandishi wa neno LIVE kwa Kiswahili sanifu
Kuna wanaoandika MBASHARA mfano TBC. Hawa jamaa mwanzoni nilidhani wamekosea tu katika typing lakini kumbe wapi, ni staili yao. Ni sawa na mtu aandike STAKI badala ya SITAKI eti kisa tu katika matamshi watu hutumia "staki"
Kuna wanaoandika MUBAASHARA na hawa si wengine bali ni Imaan media. Hawa wanachanganya kiarabu na Kiswahili kiasi kwamba wanaharibu maneno ya Kiswahili kwa kulazimisha kuyatamka/kuyaandika kwa matamshi ya kiarabu. Uharibifu umeanzia kwenye jina lao lenyewe ambapo badala ya IMANI wamejiita IMAAN
Kuna wanaoandika MUBASHARA mfano ITV na hawa nadhani ndo waasisi wa kuandika na kutumia neno hili katika media. Ukiangalia kwenye lugha hawa ndio wapo sahihi zaidi