Usiwe na muhali mkuuWewe ni tafsiri halisi mpumbavu
Umeandika bandiko lote kwa kiswahili kwa kutumia maneno mengi ya kiarabu, nyinyi walugaluga wa vijijini mnatia kinyaa, mnataka tuanze kuongea lugha zetu za maporini
Halafu unaonekana una vinasaba vya ulokole
Kiswahili maneno mengi yameingiliana na kiarabu"Moja kwa moja " Ni maneno matatu tunataka neno moja😃
Hicho ni kiingereza.Laivu
Mimi pia naisikiliza sana tbcRedio ya wazee hiyo. Mimi ndiye Mzee pekee nisiyesikiliza TBC.
Ujumbe ni ujumbe tu mkuu. Ukiwa mmoja ni ujumbe ukiwa zaidi ya mmoja ni ujumbe pia.Jumbe zikiwa nyingi
Ujumbe ukiwa mmoja
Neno zuri na ambalo kwangu mimi naona linarahisha ni ''live''. Lingetumika tu neno ''live'' kuliko kuanza tena kutunga maneno yenye asili ya kigeni. Kama wanasema ''live'' ni neno la kigeni, je, ''mubashara'' ni la kwetu? Tukope neno la kiingereza ambalo tulikuwa tumeshalizoea.Kwanini lisitumike neno lenye asili ya kibantu kama 'Moja kwa Moja' ambalo kila mtanzania kuanzia kijijini hadi mjini ataelewa maana yake?
Kuna maneno mengi ambayo tunaongea lakini wataalam wanasema siyo sahihi. Kwa mfano ''mapungufu'' (upungufu), ''lisaa limoja'' (saa moja). Na mwisho kuna ''yaliyobuniwa'' na yameshazoeleka. eg Andrew Chenge kaingiza neno lake ''makandokando''.Ujumbe ni ujumbe tu mkuu. Ukiwa mmoja ni ujumbe ukiwa zaidi ya mmoja ni ujumbe pia.
Hii ni kwa mujibu wa BAKITA.
Si unajua vijana hawa wa alfu mbili wanataka wafundishwe Kila kitu!Au kwanini mleta mada asiangalie tu tv bila kusoma hilo neno linalomkera?
TV za kireno wao huandika DIRECTO yaani Direct kwa kiingereza lenye maana sawa na hili la kiswahiliKwanini lisitumike neno lenye asili ya kibantu kama 'Moja kwa Moja' ambalo kila mtanzania kuanzia kijijini hadi mjini ataelewa maana yake?
Poor Brain, anasema wanaosikiliza TBC Kuna uwezekano mkubwa ni wachawi.Mimi pia naisikiliza sana tbc
Kweli kabisa. Wataalamu wa kiswahili wanakazi kubwa ya kufanya maneno sahihi ya kiswahili yatumike katika shughuli za kila siku hasa shughuli rasmi. Ni kazi ngumu sana.Kuna maneno mengi ambayo tunaongea lakini wataalam wanasema siyo sahihi. Kwa mfano ''mapungufu'' (upungufu), ''lisaa limoja'' (saa moja). Na mwisho kuna ''yaliyobuniwa'' na yameshazoeleka. eg Andrew Chenge kaingiza neno lake ''makandokando''.
we ni mtangazaji wa tv imaan? Naona povu linakutoka tu!Wewe ni tafsiri halisi mpumbavu
Umeandika bandiko lote kwa kiswahili kwa kutumia maneno mengi ya kiarabu, nyinyi walugaluga wa vijijini mnatia kinyaa, mnataka tuanze kuongea lugha zetu za maporini
Halafu unaonekana una vinasaba vya ulokole
we huoni kuwa kuna mkanganyiko wa mbashara, mubaashara na mubashara?Au kwanini mleta mada asiangalie tu tv bila kusoma hilo neno linalomkera?
Hakuna uchawi kuna baadhi ya vipindi huwezi kuvipata popote pale,mfano kipindi cha Manju Masoud Masoud akielezea muziki ni nani hapa afrika mashariki anaweza kushindana naye?Vipindi vya kuchekesha kama mahoka au pwagu na pwaguzi ni wapi unaweza kuvipata?Poor Brain, anasema wanaosikiliza TBC Kuna uwezekano mkubwa ni wachawi.
Mzee mwenzangu, umenena vyema sana! Yaani uchambuzi wa muziki unaofanywa na manju wa muziki Masoud Masoud ni WA kiwango kikubwa mno na huwa naufurahia sana.Hakuna uchawi kuna baadhi ya vipindi huwezi kuvipata popote pale,mfano kipindi cha Manju Masoud Masoud akielezea muziki ni nani hapa afrika mashariki anaweza kushindana naye?Vipindi vya kuchekesha kama mahoka au pwagu na pwaguzi ni wapi unaweza kuvipata?
Kipindi cha mbazigwa hassan na tshimanga assossa unaweza kuvipata wapi?
Unajua usidhani kuwa sisi tunaosikiliza redio tunafata siasa,la hasha tunafata vipindi vizuri,utangazaji wenye kuzingatia maadili na taarifa zilizohaririwa vizuri
Siku hizi taasisi nyingi wamejazwa chawa.Ujumbe ni ujumbe tu mkuu. Ukiwa mmoja ni ujumbe ukiwa zaidi ya mmoja ni ujumbe pia.
Hii ni kwa mujibu wa BAKITA.
BAKITA inakazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania kwa sababu kwa njia wanaotumia ni ngumu sana kuwafikia watanzania wengi.Siku hizi taasisi nyingi wamejazwa chawa.
BAKITA nao ni hovyo tu ndio maana siku hizi matumizi ya X yameshamiri kwenye maandishi ya kiswahili. Bado kidogo Q nayo itaanza kutumika.
Matumizi sahihi ya H, L na R pia hakuna. Zamani kutojua kutofautisha R na L lilikuwa tatizo la wakurya lakini kwasa a a ni nchi nzima hadi mashuleni. BAKITA wanakodoa macho tu
Kwenye Jina mtu hapangiwi namna ya kujiita. Hata wangejiita EMAN, IMANI kwa sababu ni jina. Ndio maana kuna MUHAMMAD, MOHAMED, MOHAMMED, MOHAMEDI maana na lengo ni moja kila mtu ameamua design yake, pia kuna Ally na Ali, kule Afrika Magharibi kuna Aliou, wapo pia wanaojiita Aliyyu. Wote reference yao ni moja.Ukiangalia kuna chaneli kama makundi matatu hivi juu ya uandishi wa neno LIVE kwa Kiswahili sanifu
Kuna wanaoandika MBASHARA mfano TBC. Hawa jamaa mwanzoni nilidhani wamekosea tu katika typing lakini kumbe wapi, ni staili yao. Ni sawa na mtu aandike STAKI badala ya SITAKI eti kisa tu katika matamshi watu hutumia "staki"
Kuna wanaoandika MUBAASHARA na hawa si wengine bali ni Imaan media. Hawa wanachanganya kiarabu na Kiswahili kiasi kwamba wanaharibu maneno ya Kiswahili kwa kulazimisha kuyatamka/kuyaandika kwa matamshi ya kiarabu. Uharibifu umeanzia kwenye jina lao lenyewe ambapo badala ya IMANI wamejiita IMAAN
Kuna wanaoandika MUBASHARA mfano ITV na hawa nadhani ndo waasisi wa kuandika na kutumia neno hili katika media. Ukiangalia kwenye lugha hawa ndio wapo sahihi zaidi