Neno Mubashara: Chaneli ya taifa mnaharibu lugha, chaneli ya dini na nyinyi amueni moja mtumie kiswahili ama kiarabu

Neno Mubashara: Chaneli ya taifa mnaharibu lugha, chaneli ya dini na nyinyi amueni moja mtumie kiswahili ama kiarabu

Niliwasikia masheikh wanaopinga maandamano wanasema "majambo" mbalimbali badala ya "mambo" mbalimbali kidogo nipasue kiio cha iphone 17.
 
Wewe ni tafsiri halisi mpumbavu
Umeandika bandiko lote kwa kiswahili kwa kutumia maneno mengi ya kiarabu, nyinyi walugaluga wa vijijini mnatia kinyaa, mnataka tuanze kuongea lugha zetu za maporini
Halafu unaonekana una vinasaba vya ulokole
Usiwe na muhali mkuu
 
Kwanini lisitumike neno lenye asili ya kibantu kama 'Moja kwa Moja' ambalo kila mtanzania kuanzia kijijini hadi mjini ataelewa maana yake?
Neno zuri na ambalo kwangu mimi naona linarahisha ni ''live''. Lingetumika tu neno ''live'' kuliko kuanza tena kutunga maneno yenye asili ya kigeni. Kama wanasema ''live'' ni neno la kigeni, je, ''mubashara'' ni la kwetu? Tukope neno la kiingereza ambalo tulikuwa tumeshalizoea.
 
Ujumbe ni ujumbe tu mkuu. Ukiwa mmoja ni ujumbe ukiwa zaidi ya mmoja ni ujumbe pia.

Hii ni kwa mujibu wa BAKITA.
Kuna maneno mengi ambayo tunaongea lakini wataalam wanasema siyo sahihi. Kwa mfano ''mapungufu'' (upungufu), ''lisaa limoja'' (saa moja). Na mwisho kuna ''yaliyobuniwa'' na yameshazoeleka. eg Andrew Chenge kaingiza neno lake ''makandokando''.
 
Au kwanini mleta mada asiangalie tu tv bila kusoma hilo neno linalomkera?
Si unajua vijana hawa wa alfu mbili wanataka wafundishwe Kila kitu!

Sisi wa zamani tulipokuwa na wazazi wetu (pamoja), halafu jagoo akampanda kuku tulikuwa hatuangalii tukio lile kwa sababu linakera, badala yake tunaanzisha story zisizo na kichwa Wala miguu ili kuupotezea mtanange wa kuku.

Vijana wajiongeze bhana Ili wasikerwe na Kila kitu, la sivyo watakumbwa na ugonjwa wa akili.
 
Kwanini lisitumike neno lenye asili ya kibantu kama 'Moja kwa Moja' ambalo kila mtanzania kuanzia kijijini hadi mjini ataelewa maana yake?
TV za kireno wao huandika DIRECTO yaani Direct kwa kiingereza lenye maana sawa na hili la kiswahili
 
Kuna maneno mengi ambayo tunaongea lakini wataalam wanasema siyo sahihi. Kwa mfano ''mapungufu'' (upungufu), ''lisaa limoja'' (saa moja). Na mwisho kuna ''yaliyobuniwa'' na yameshazoeleka. eg Andrew Chenge kaingiza neno lake ''makandokando''.
Kweli kabisa. Wataalamu wa kiswahili wanakazi kubwa ya kufanya maneno sahihi ya kiswahili yatumike katika shughuli za kila siku hasa shughuli rasmi. Ni kazi ngumu sana.

Eti wanasema neno 'maamuzi' si sahihi, badala yake tutumie neno 'uamuzi'.
 
Wewe ni tafsiri halisi mpumbavu
Umeandika bandiko lote kwa kiswahili kwa kutumia maneno mengi ya kiarabu, nyinyi walugaluga wa vijijini mnatia kinyaa, mnataka tuanze kuongea lugha zetu za maporini
Halafu unaonekana una vinasaba vya ulokole
we ni mtangazaji wa tv imaan? Naona povu linakutoka tu!
 
Poor Brain, anasema wanaosikiliza TBC Kuna uwezekano mkubwa ni wachawi.
Hakuna uchawi kuna baadhi ya vipindi huwezi kuvipata popote pale,mfano kipindi cha Manju Masoud Masoud akielezea muziki ni nani hapa afrika mashariki anaweza kushindana naye?Vipindi vya kuchekesha kama mahoka au pwagu na pwaguzi ni wapi unaweza kuvipata?
Kipindi cha mbazigwa hassan na tshimanga assossa unaweza kuvipata wapi?
Unajua usidhani kuwa sisi tunaosikiliza redio tunafata siasa,la hasha tunafata vipindi vizuri,utangazaji wenye kuzingatia maadili na taarifa zilizohaririwa vizuri
 
Mzee mwenzangu, umenena vyema sana! Yaani uchambuzi wa muziki unaofanywa na manju wa muziki Masoud Masoud ni WA kiwango kikubwa mno na huwa naufurahia sana.

Dah, siku moja alimwelezea mwanamuziki wa zamani wa Tanzania aliyetamba hapa nchini na nje ya nchi na pia kutambuliwa na mwalimu J.K Nyerere, Ubi Ukwe Zawose hadi raha.

Kwa kweli Masoud Masoud, aongezewe miaka mingi ili wazee tupate kufaidi uchambuzi tukuka wa muziki.

Hivi mchezo wa Pwagu na Pwaguzi Bado unarushwa pale TBC?

Dr am 4 real PhD.
 
Ujumbe ni ujumbe tu mkuu. Ukiwa mmoja ni ujumbe ukiwa zaidi ya mmoja ni ujumbe pia.

Hii ni kwa mujibu wa BAKITA.
Siku hizi taasisi nyingi wamejazwa chawa.

BAKITA nao ni hovyo tu ndio maana siku hizi matumizi ya X yameshamiri kwenye maandishi ya kiswahili. Bado kidogo Q nayo itaanza kutumika.

Matumizi sahihi ya H, L na R pia hakuna. Zamani kutojua kutofautisha R na L lilikuwa tatizo la wakurya lakini kwasa a a ni nchi nzima hadi mashuleni. BAKITA wanakodoa macho tu
 
BAKITA inakazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania kwa sababu kwa njia wanaotumia ni ngumu sana kuwafikia watanzania wengi.

Kuwaelimisha watu kupitia vipindi vya Redio na TV pekee ni ngumu mno.

Tusubiri tuone.
 
Ukiangalia kuna chaneli kama makundi matatu hivi juu ya uandishi wa neno LIVE kwa Kiswahili sanifu

Kuna wanaoandika MBASHARA mfano TBC. Hawa jamaa mwanzoni nilidhani wamekosea tu katika typing lakini kumbe wapi, ni staili yao. Ni sawa na mtu aandike STAKI badala ya SITAKI eti kisa tu katika matamshi watu hutumia "staki"

Kuna wanaoandika MUBAASHARA na hawa si wengine bali ni Imaan media. Hawa wanachanganya kiarabu na Kiswahili kiasi kwamba wanaharibu maneno ya Kiswahili kwa kulazimisha kuyatamka/kuyaandika kwa matamshi ya kiarabu. Uharibifu umeanzia kwenye jina lao lenyewe ambapo badala ya IMANI wamejiita IMAAN

Kuna wanaoandika MUBASHARA mfano ITV na hawa nadhani ndo waasisi wa kuandika na kutumia neno hili katika media. Ukiangalia kwenye lugha hawa ndio wapo sahihi zaidi
Kwenye Jina mtu hapangiwi namna ya kujiita. Hata wangejiita EMAN, IMANI kwa sababu ni jina. Ndio maana kuna MUHAMMAD, MOHAMED, MOHAMMED, MOHAMEDI maana na lengo ni moja kila mtu ameamua design yake, pia kuna Ally na Ali, kule Afrika Magharibi kuna Aliou, wapo pia wanaojiita Aliyyu. Wote reference yao ni moja.

Imaan wanataka wewe utamke jina lao kwa Kiarabu sahihi, sio kosa.
Ila neno Mubashara hapo nakuunga mkono, hilo neno hawawezi kutuamulia namna ya kutamkwa.
 
Back
Top Bottom