Netanyahu aapa kujenga Ukuta Jordan kuzuia Wahamiaji wa Kiafrika, waliopo kuondolewa Israel

Netanyahu aapa kujenga Ukuta Jordan kuzuia Wahamiaji wa Kiafrika, waliopo kuondolewa Israel

Hapa unaongelea sababu ya waafrika kukimbilia ulaya au Waafrika kuoga tamaduni za wazungu/waarab? Kwa vyovyote viongozi wanahusika ndiyo maana hata DP inatetewa kidini na viongozi wanafurahia
Vyote si hamna chenu ndio maana mnatangatanga hovyo
 
Huu uzi hawatokuja kushabuliwa kwa sababu Gallatians ni machawa wa Israeli na Mayahudi ,ila angekuwa Muarabu hapa matusi na dhihaka zingetawala...View attachment 2738466
We adriz unajua kabisa hawa ni wajasiriadini na wala siyo mitume wala manabii. Huwezi kutumia ofisi ya chizi kama huyu kusema Wakristu ni machawa wa Wayahudi/Israel
 
Nafikiri hata weusi tukihamishiwa wote Ulaya na weupe wote waje Africa!!😳
Bada ya miaka mingi itakayopita weusi wataanza tena kuzamia Africa!😂

Weusi waaribifu, wabadhirifu, wezi na hawafikirii wengine wala miaka ijayo huangalia kesho na familia zao basi!!

Kuzamishwa baharin na kujengewa kuta haya yote ni kutokana na kujulikana kwa athari zao😳😳

NB: mi mweusi pia😂😂😂
 
Huu uzi hawatokuja kushabuliwa kwa sababu Gallatians ni machawa wa Israeli na Mayahudi ,ila angekuwa Muarabu hapa matusi na dhihaka zingetawala...View attachment 2738466
images (1).jpeg
 
Ukimuona adriz Accumen Mo na Kikwajuni One wanavyotamani kuwa waarabu
😂😂Sisi ni independents ndo maana hata viongozi wetu hwachaguliwi Vatican na uingereza kama nyie...
Wala hatufuati matamko na wala hatuna mpango wa kuishi nje .


Popote pale tunaweza kuabudu kikubwa Qibla direction na maandiko ni yale yale hayawezi kuharibiwa wala kubadilishwa.
 
Sasa wanaowasumbua Israel ni waislamu wa kiarabu halafu wawachie tena waarabu chotara wa Eritrea ambao ndio waislamu wa imani kali kuliko Hamas? Hata kama ni wewe ungekubali watu ambao unajua kabisa watakuja kuwa mwiba kwako baadaye waje nchini mwako?

Itoshe tu kusema afadhali wazungu kuliko waarabu
 
Licha ya kujipendekeza kwenye dini za Wazungu/Waisrael (Christian) na Waarabu (Islam) Bado mtu Mweusi anakataliwa Kila mahala.

Ikumbukwe Morocco na Tunisia zilisema zitawatimua Watu Weusi wote na Kuzuia kuingia Nchini humo.

Huko Ulaya maelfu hufa maji na huachwa waozee huko na Wazungu wanapojaribh kuvuka Kwa magendo kwenda Ulaya.

Swali:
Kwa nini Mtu mweusi anakataliwa Kila sehemu? Je, kuna disorder sehemu au?

=======

ISRAEL, Tel Aviv: Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kujenga ukuta mwingine wa mpaka - wakati huu kwenye mpaka wa mashariki wa nchi hiyo na Jordan - ili kuwazuia wahamiaji ‘haramu’ kutoka nchi za Afrika wanaofurika kuomba hifadhi.

"Tuliweka uzio kwenye mpaka wetu wa kusini (Misri) na kusimamisha uingiaji kutoka huko hadi Israeli," Netanyahu alisema katika taarifa yak. "Kwa hivyo tulisimamisha zaidi ya waingiaji milioni 1 kutoka Afrika, ambao wangeharibu nchi yetu. Sasa tutajenga uzio kwenye mpaka wetu wa mashariki (Jordan) na kuhakikisha kwamba hakutakuwa na upenyaji kupitia huko."

Kiongozi huyo wa Israel ametoa kauli yake baada ya kuitisha mkutano maalum wa mawaziri wake katika kukabiliana na ghasia kubwa zilizowahusisha wahamiaji wa Eritrea siku ya Jumamosi mjini Tel Aviv. Alitoa wito kwa mawaziri wake kuandaa mipango mipya ya kuwafukuza sio tu raia wa kigeni waliohusika katika ghasia za wikendi hii, bali pia wahamiaji wengine wa Kiafrika.

Serikali ya Netanyahu ilikataa kutoa hadhi ya ukimbizi ya waomba hifadhi wengi wa Kiafrika, ikiwataja kama "waingiaji haramu." Nchi hiyo inaripotiwa kuwa na wahamiaji wapatao 25,000, wakiwemo 18,000 kutoka Eritrea. Wengi wao waliingia Israeli kinyume cha sheria kwa kuvuka Peninsula ya Sinai ya Misri. Ukuta wa mpaka wa kusini wa Israel ulikamilika Desemba 2013, na kusababisha kupungua kwa kasi ya wahamiaji haramu nchini humo.

"Tutalinda mipaka yetu," Netanyahu alitangaza Jumapili. "Tutailinda nchi yetu."
Kwanini hao wapumbavu wasiwekewe ukuta? Wameenda kuomba asylum, wengine wamezamia tu lakini wakaachwa waendelee kujitafutia.
Matokeo yake mabifu ya nyumbani kwao wameenda kuyafanyia nchi za watu.
Hapa kwenye video ni vurugu zilizotokea huko Tel Aviv ambapo makundi mawili yalipigana kuumizana na kusababisha uharibifu.
Kundi la kwanza ni asylum seekers waliokua wakiandamana kuipinga serikali ya Eritrea, likatokea kundi la pili ambalo liliposikia kuwa kutakua na maandamano ya kuipinga serikali lenyewe likajiandaa kuwakabili hao wanaoipinga serikali na ndipo mapigano makubwa yakaibuka, ni mapigano yaliyomwaga sana damu.
Netanyahu kaitisha Cabinet na kuwataka mawaziri wamletee mpango wa kuwarudisha nyumbani zaidi ya asylum seekers 1,000.
Wachambuzi wakamkosoa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria kurudisha asylum seekers nchini kwao.
Netanyahu amewajibu kuwa hakuna sheria inayovunjwa kwa kuwarudisha hao asylum seekers zaidi ya 1,000 sababu kama wao wanaiunga mkono serikali yao, maana yake hawana cha kuhofia kuishi nchini mwao. Hivyo lazima warudishwe.
 
🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom