ITR
JF-Expert Member
- Sep 22, 2022
- 6,096
- 16,390
Kinacho muweka njia panda Netanyau ni jinsi ya kulinda madaraka yake na sio malengo ya vita ndani ya gaza.Ni kweli lakini Netanyahu anakuwa njia panda kwa sababu Hamas wanasema hakuna deal lolote bila IDF kuondoka Gaza na vita kuisha, kitu ambacho Netanyahu hataki na anaona kama ni kuwapa ushindi hamas.
Kuhusu mateka ni kwamba inaonekana wanakuwa na taarifa ya baadhi wa mateka walipo na wanashindwa kuchukua hatua kwa kuogopa hasara kama iliyotokea jana. Kwa sababu wanasema operation ya jana ilikuwa approved tangu Alhamis na inaonekana imefanyika kama kuwashinikiza hamas kukubal deal.
Shida Netanyahu aliweka malengo ambayo kwa sasa ynamuweka njia panda.
Anajua kabisa kuwa vita ikiisha hatakuwa na namna nyingine ya kulinda madaraka yake.
Hii vita inaigharimu sana Israel kiuchumi na kidipromasia na ndio maana baadhi ya wanasiasa ndani ya Israel wanataka ifike mwisho.
Tena baadhi ya wanasiasa ndani ya Israel kwenyewe wanamlaumu Netanyau kuwa ndo chanzo cha kuichochea Hamas atekeleze shambulizi la October 7 kwa sababu ya sera zake dhidi ya wapalestina.