Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Njama dhidi ya Palesina,Gaza na Hamas zimeshindwa vibaya mpaka sasa kiasi kwamba wahusika wakuu kutoka Marekani na Israel wamekuwa wakiropokwa ovyo.
Raisi Trump wiki mbili zilizopita alitoa ya moyoni yaliyokuwa wameyaficha pale aliposema anataka awahamishe wapalestina na kupajenga upya Gaza.Jambo hili liliwahi kuelezwa mwanzoni mwa vita kwamba Israel ilikuwa na mpango wa kuwahamisha wapalestina kwa ujanja waende Sinai.
Trump katika maelezo yake na kwa kujiamini akasema angewaeleza mfalme Abdallah wa Jordan na raisi Sisi wa Misri ii wawachukue wapalestina wa Gaza. Mbali na viongozi kadhaa wa dunia kushangazwa na tamko hilo viongozi hao wa Jordan na Misri nao walikataa suala hilo. Kuona hivyo Trump akaamua afiche uso wake kidogo japo nia ni hiyo hiyo.
Mara baada ya kuzungumza na Netanyahu naye akarudi na ari mpya ya kuendeleza mpango huo na juhudi mpya na vitisho akaviongeza.
Mark Rubio ambaye amechukua nafasi iliyokuwa ya Blinken katika ziara zake mpya za mashariki ya kati amenuna na kukataa kuzitembelea nchi za Jordan na Misri na badala yake akazungumza na Netanyahu na kudhihirisha kwamba wao wameshindwa kupambana na Hamas.
Rubio akasema jukumu hilo la kupambana na Hamas lichukuliwe na mataifa ya kiarabu kama vile Misrii ili wawashinde Hamas na kuunda serikali itakayoendeshwa na wao bila Hamas.Katika malalamiko yake akizungumza na Netanyahu Rubio alisema kila kitu kitakuwa kigumu kwani Hamas bado wana bunduki.
Ufupisho wa maneno ni kuwa Hamas na wapalesdtina imekuwa ni kaa la moto kwa Trump na Netanyahu.
Wangependa wawamalize na kuendelea na mpango wao walioufichukua lakini tatizo jee ni wapi watawapeleka.