Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Imebaki siku moja tu kabla ya kuonyeshwa duniani kote, Netflix wameachia trela ya kwanza kabisa ya Sean Combs: The Reckoning, mfululizo wa documentari ya sehemu nne (four-part docuseries) iliyosimamiwa na kutayarishwa na Curtis “50 Cent” Jackson. Series hii inatarajiwa kudondoshwa kesho, Disemba 2, 2025, na imetua kwa wakati mbaya zaidi: Wakati Sean “Diddy” Combs yuko mikononi mwa serikali ya Marekani akisubiri kesi kwa mashtaka mazito za kupanga njama za sex trafficking, na usafirishaji wa watu kwa biashara ukahaba.
Trela hiyo ya dakika mbili za kushtua, Inaanza na picha za zamani (archival footage) za Puff Daddy akitabasamu na kuparty miaka ya ’90 (Bad Boy Records ikiwa kileleni, private jet, na mvua ya champagne) kabla ya kukatika ghafla na kuonyesha klipu ya interview ya Combs mwenyewe ya mwaka 2023 akisema, “Ukipata power (nguvu), watu wanataka kukupokonya… wakati mwingine, watu wa karibu ndio watakaokugeuka.” Screen inabadilika na kujaa vichwa vya habari (headlines) vya kesi chungu nzima, video ya Cassie hotelini ya 2016, uvamizi wa ‘Homeland Security’ kwenye nyumba zake, na mwisho kukamatwa kwake Septemba 2024.
Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, 50 Cent amekuwa akimchokonoa sana Diddy huko mitandaoni, anajitokeza mara mara kamera kwa mara ya kwanza kwenye trela, akitoa sentensi moja tu ya kikali ambayo tayari imekuwa trending/viral: “Nimekuwa nikiwaambia kwa miaka mingi… kuna mambo hayawezi kurudi nyuma.”
Bifu kati ya hawa jamaa limeanza miaka ya 2000, ambapo walikuwa wakitupiana vijembe vya chini chini juu ya biashara zao na unaa wa kitaani. Baada ya kesi ya Cassie Ventura ya 2023 na mfululizo wa madai mengine (zaidi ya kesi za madai 30 zikimtuhumu Combs kwa unyanyasaji wa kingono, ukatili wa kimwili), 50 Cent alitumia nafasi hiyo kuendeleza chokochoko zake. Disemba 2023 alitangaza kuwa anaandaa documentari kuhusu kashfa hizo, akiahidi mapato yote yatakwenda kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono. Baada ya kugombaniwa sana na makampuni, inasemekana Netflix walilipa mamiloni ya hela kununua project hiyo.
Mapokeo ya Documentary hii huko mitandaoni yamekuwa ya mitazamo mbalmbali. Trela ilipata watazamaji milioni 18 kwenye mitandao mbalimbali ndani ya masaa sita tu. Maoni yametofautiana kutoka “50 Cent ni ultimate troll (mchokozi aliyeshindikana) aliyegeuka kuwa mleta kweli” hadi tuhuma juu ya documentray hiyo inafanya biashara kwa kutumia maumivu ya wengine. Moja suala linalojirudia rudia ni hili lakusema “Amegeuza bifu kuwa mradi wa mabilioni ya dollar.”
Series hii imeongozwa na Emmy, Nadia Hallgren (Becoming), na inaahidi kuonesha picha ambazo hazijawahi kuonekana, ikiwemo mahojiano na wasanii wa zamani wa Bad Boy, wadau wa tasnia ya Mziki, vyanzo kutoka vyombo vya dola, na baadhi ya watu wanaomtuhumu Combs (baadhi wamejitokeza bila kutajwa majina). Netflix wanaielezea kama “uchunguzi usio na woga kuhusu nguvu, umaarufu, na upande wa giza wa American music industry.”
Pamoja na kesi ya jinai ya Combs kuanza rasmi Mei 2025 na kesi mpya za madai zikiendelea kufunguliwa kila wiki, Timing ya kuachia documentari hii unaweza kuwa kaa la moto kwa ndugu Diddy.
Waandaaji wa The Reckoning wanataka makala hiyo ikumbukwe kama uandishi wa habari za uchunguzi, kisasi cha shambulio la aibu kati mahasimu wa muda mrefu, au vyote viwili kwa pamoja.
Kesho usiku, Server za Netflix zitakuwa busy sana kuhudumia mamlioni ya watu waliokuwa wakiisubiri makala hii.
Sean Combs: The Reckoning itaachiwa Netflix Disemba 2, 2025.