Netflix imekubali kuinunua kampuni ya filamu na kurusha maudhui ya Warner Bros Discovery kwa dola za kimarekani Bilioni 72. Netflix ameibuka kinara wa zabuni ya kuinunua Warner Bros baada ya kuwapiku washindani wake Comcast na Paramount Skydance baada ya vita kali.
Tume ya ushindani ikipitisha mauzo hayo inatarajiwa kutengeneza kampuni kubwa sana kwenye sekta ya filamu huku baadhi wakipinga wakihofu kupanda kwa bei na walaji kukosa ladha tofauti.
Anyways nimegundua mataifa yetu ya dunia ya tatu bado maskini kuliko nilivyofikiri kama ukwasi wa kampuni moja ya Kimarekani inaweza kufix deni linalotusumbua tangu tumezaliwa na kila leo linaandikwa kwenye vichwa vya habari na kuibuka kwenye mijadala ya Bunge.. ni kikao kimoja tu cha bodi kingeliondoa na bajeti ya mwaka mzima kama bonus bila wahisani kuchangia.