Awali ya yote mimi ni muoga wa vyombo vya usafiri (ndege, bus na pikipiki).
Nilivyokua nikisoma zile habari za magari ya magazeti au malorry nilikua nashangaa mtu anapata emergency gani ya kupanda hayo mausafiri.
Leo sasa yamenigeukia. Nimefika Singida saa mbili kasoro bus tulilopanda wakaleta ubabaifu hivyo ikabidi watutafutie usafiri mwingine na hapo mwanamke niko peke yangu na wanaume watatu.
Mara yakaja haya malorry marefu ya mizigo halafu kuna nafasi mbili tu moja nikapanda mimi nyingine akapanda mkaka anaenda Dar.
Nilivyoingia kwenye lile gari moyoni nikawa najisemea never say never. Kweli mimi leo ni wa kupanda haya madude? Hapo umamaduu wote nimeweka pembeni nawaza nifike Dom tu nikalale.
Kwa uoga nikaanza kusweat viganjani. Nikaanza kukumbuka yanavyoangukaga na kuua. Nikaanza kumuwaza mwanangu. Nikawa nasali tu salamu Maria. Nikampigia simu bby nimueleze usafiri niliopanda. Akanitisha vya kutosha oooh wanaweza kukubaka Mara wakuchinje usiku huu bora ushuke utafute sehemu ulale uendelee na safari kesho. Kama Mungu hatukua mbali na mji nikawaomba wasimamishe gari nikashuka.
Hapa nipo kwenye guest house vumbi kama lote. Najua asubuhi nitaamka na mafua ya kutosha ila bora nitapanda bus mchana nikiwa na amani.
Never say never sababu mimi sikutegemea ipo siku nitapanda lorry japo nimeshindwa kuvumilia kumaliza safari
Sent using
Jamii Forums mobile app