Oktoba 13, 2019
KANALI MSTAAFU LUBINGA: WAKO WALIOTAKA HATA NYERERE ASING'ATUKE
Katibu wa Siasa na Uhusiano kimataifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kanali mstaafu Ngemela Lubinga akifanyiwa mahojiano na Khalifa Said kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa na masuala mtambuka ya siasa za ndani ya Tanzania
Kumekuwa na maoni kwamba hoja na ushawishi unaofanywa na baadhi ya wananchi kutaka ukomo wa uraisi uondolewe katika Katiba, unaweza kumfanya Raisi John Magufuli ashawishike na hivyo kuchukua hatua za kubaki madarakani wakati muda wake utakapoisha.
Katika sehemu hii ya MCL Talk, mwandishi Khalifa Said anafanya mahojiano na Kanali Ngemela Lubinga, anayehusika na siasa na uhusiano wa mambo ya nje ya Chama cha Maapinduzi (CCM) akitaka kufahamu kwamba katika muktadha kama huo, wao kama chama wana uhakika gani kwamba mwenyekiti wao ataheshimu Katiba na kuondoka madarakani muda wake utakapoisha?
Source : Mwananchi digital