New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Hoja ya kudai kifungu namba 13 kinamhitaji Mwekezaji aendeleze ujuzi wa wafanyakazi halina namna likapimika



Ana waendeleza ili iwe nini?


Kwani yeye mkataba unamtaka awaandae TPA ili waje kuendesha hilo kampuni au kapewa fursa ya kuwadhoofisha hadi wafe?

Haya malengo ya kuwaimarisha TPA yana mgongano na mkataba mzima ulivyo.
 
Ikija kutangaza matokeo ya chaguzi huchukua wiki mbili ukiuliza wanasema nchi ni kubwa ikija bunge kukusanya maoni ya wananchi wachangie juu ya mkataba feki muda ni siku moja


Hakuna anayekumbuka nchi ni kubwa na haiwezekani watu watoke mikoani hadi wafike Dodoma na kuweza kufikisha michango yao.


Hapa ndipo tulipofikia
 


Tatizo kubwa la haya mawazo mgando ni kuweka mbele ufanisi bila kutafakari thamani endelevu ya uhuru wa kujitawala.

Inatosha kukumbushana jukumu kuu la serikali ni kutoa huduma na siyo kufanya biashara. Serikali yoyote ile ambayo inakasimu jukumu lake la usalama wa taifa halina uhalali wa kuendelea kutawala.

Tz hatujawekeza bandarini kama walivyowekeza Dubai. Kweli kuikana katiba yetu kwa uwekezaji wa $600 Mill ambazo ni kiduchu inathibitisha uwezo wa kufikiri wa mtanzania ulipogota. We name it as poverty mentality.

Sisi siyo Rwanda au nchi nyingine zinazowapa mataifa mengine ardhi wawafanyie wao kazi. Kazi tutafanya wenyewe siyo askari wa mamluki

Nchi zote zenye maendeleo zimeamini watu wao na kuwawezesha wakati sisi tunafungua fursa kwa mamluki.

Uzuri migogoro inakuja. Baada ya 2030 Rais atakayekuja atatengua huu mkataba. Na utashangaa wabunge hawahawa watalipitisha hilo azimio
 
Bunge la JMT limekiri limeshindwa kutunga sheria pale lilipoamua uuzwaji wa bandari zetu zote usisimamiwe na sheria zetu bali usimamiwe na sheria za mkoloni wa kiingereza.


Kutokana na huu ukweli, wazo na mikakati ya kuliuza bunge kwa waingereza ili warudi upya na kutunga sheria lina mashiko maana TPA imeporwa mamlaka ya kisheria kwa sababu za utendaji mbovu na sababu hizi hizi pia bunge linahusika.
 
Serikali hii yote iliapa kulinda na kutetea katiba yetu kwa kukubali kwao uuzwaji wa bandari zetu kwa waarabu na sheria za uingereza zitumike ni kuisigina katiba yetu kwa hiyo kwa umoja wao wameviasi viapo vyao na hivyo kupoteza uhalali wa kutawala na wawe waungwana wajiuzulu.


Tufike mahali tufute viapo maana watu wanaapa bora liende lakini hawana hata nia ndani ya mioyo yao kutii hivyo viapo.

Na ndiyo maana Maandiko yanatuagiza tusiape kwa sababu hatutavitii hivyo viapo na hivyo kuongeza uadui tu na Mwenyezi Mungu.
 
Wale mnaomsifia Mwendazake (JPM) mkumbuke sababu kuu hii serikali imetuingiza mkenge ni kwa sababu ya mazingira aliyoyajenga mwenyewe ya kuiba kura chaguzi za 2020 na hivyo tukawa na uwakilishi haramu ambao hauwajibiki kwa wapigakura bali unawajibika kwa CCM ambao ndiyo waliwachagua.

Uwakilishi haramu ndiyo unazaa hulka ya kuupinga utawala wa sheria maana hauwajibiki kwa wananchi na hapa ndipo tumegota.
 
Nina uhakika bila shaka, NGOs nyingi wako kwenye mikakati ya kuwaburuza hawa wakora mahakamani.

Okoeni muda na vijisenti vyenu msiende huko maana mahakama zetu teuzi zake zina macho na wengi wa hao waheshimiwa ni makada wa CCM.

Wamebebwa ili kulinda dhuluma na mkienda huko watanukuu hukumu ya kifisadi ya Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu inayosema kama Bunge lina koramu mahakama haiwezi kutengua maamuzi yao.

Kwa lugha nyingine, kama Bunge lina koramu likaamua majaji wote wachinjwe itabidi tu wachinjwe na hata kama kesi itakuja mbele ya hawa waheshimiwa watakuwa hawana jinsi bali kuamua hawana mamlaka ya kutengua maamuzi ya Bunge kwa hiyo wachinjwe tu teh teh teh.

Tunajua watatengua fasta kwa mwendokasi ambao hata nuru hautashindana nao. [emoji2] [emoji3] [emoji1] [emoji16] [emoji1787] [emoji23] [emoji2] [emoji3] [emoji1] [emoji16]

Hebu fikiria, wastaafu walipodai sheria ya mafao iliyowapora hata wale waliohitimu miaka 50 malipo yao yakasitishwa na bunge Mahakama ya Rufani ilipotengua uamuzi wa mahakama kuu wa kurejesha haki za wastaafu walisema pensheni siyo ujira hivyo hailindwi na katiba wakati mkataba wa ajira ni uleule!!!!!!!!!!!!!

Kwenye marejeo, mahakama ya rufani ikasema sheria hii mpya pamoja imekuwa mshindo nyuma (retrospectivity) haikiuki katiba wakati inakiuka.

Uamuzi huu ulilenga kuwanyima malipo ya pensheni wastaafu walio na miaka 50-55.

Pia uamuzi huu ni pigo kwa sheria ya jinai kwani sasa bunge linaweza kutunga sheria zenye adhabu kubwa kuliko za awali na kuamuru waadhibiwe hata wale ambao walitenda makosa hayo kabla ya sheria hizo mpya kutungwa na hivyo kukiuka katiba yenye makatazo ya sheria za mshindo nyuma (retrospectivity).

Tunajua sheria ya pensheni itaendelea kubadilishwa kwa kupaaishwa umri wa kustaafu kwa kuwa mifuko hii inaliwa na inatafunwa kwa sababu wafanyakazi siyo wasimamizi wa hiyo mifuko.

Wanasiasa waandamizi wa CCM ambao siyo wachangiaji wa hiyo mifuko ndiyo wanayoisimamia na hawana uchungu nayo na hivyo huifuja sasa kufidia wizi na ubadhirifu unaoendelea kwenye hiyo mifuko ni kuzuia kwa kutumia sheria wastaafu kulipwa chochote na hata kuwaombea wafe mapema ili wasije kuikausha hii mifuko.


Sasa, tulitegemea mahakama ya rufaa itende haki kwa kusema kwa vile malipo ya kustaafu ni sehemu ya mkataba wa ajira basi chochote mfanyakazi anacholipwa kinatokana na mkataba ni ujira wa mfanyakazi na unalindwa na katiba. Lakini hawa nguli wa sheria wakaona hapana malipo ya uzeeni pamoja yanatokana na mkataba wa ajira siyo mshahara maana mfanyakazi hayuko kazini.

Mbavu zangu hoi, hivi mfanyakazi anapolipwa mshahara akiwa likizo na hafanyi kazi huo siyo ujira? Kama ni ujira kwanini malipo baada ya kustaafu yasiwe ni sehemu ya ujira kama siyo dhuluma dhidi ya wastaafu wanyonge.

Mbali ya teuzi za majaji kuwa zinalenga kulinda uozo serikalini lakini pia mafao ya kustaafu ya hawa waheshimiwa yana sheria tofauti na hizi za wafanyakazi wengine na ndiyo maana hawaguswi na maamuzi yao yaliyokithiri dhuluma.

Kwa hiyo, enyi wenye NGOs mtafakari hizi hoja labda kama mna wafadhili nje ya nchi basi mna ubavu wa kufika hadi Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika maana kwenye mahakama zetu andikeni maumivu kwa haya masuala ya wazi ya kukiuka katiba ya nchi.

Vinginevyo, msijitese bure wenzenu tayari wamejipanga.
 
Tulichojifunza kwa wamarekani vuguvugu la kisiasa tu ndilo litatengua maazimio ya kibunge na mikataba feki.

Hakuna cha mikataba ya milele mbele ya nguvu ya umma.

Tutaendelea kuelimishana ili Rais ajaye wa 2030 afute huu upuuzi kama wataamua kwenda kwa msuluhishi waache waende lakini bandari zetu zitasimamiwa na makampuni ya umma ya watanzania na hakuna cha ubia bali kuongeza uwezekaji tu zaidi hata ya ATC ambako hakuna la maana linaloendelea huko.
 
Free mason is real na hao ndio wanaongoza Nchi na wanapanga mipango ya Nchi nani awe raisi nani auwawe.
 


Never forget Makinikia extrapolation, which nobody in the CCM wants to hear, let alone regurgitate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…