New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

YUKO WAPI WAZIRI MKUU KWENYE HII NGOMA?


Waziri Mkuu yuko wapi kwenye hili sakata mbona kimya chenye mshindo mkuu kuna nini?

Mgawanyiko ndani ya baraza la mawaziri au?

Asichojua 2030, hawa njemba wanajua atachukua fomu ya Urais na jina litakatwa kama la mawaziri wakuu waliotangulia.


Majina 5 ya urais ya CCM 2030 ni kwa wale wamo wanautafuna huu mzoga unaitwa DP WORLD kama haumo hawatakuamini kukuachia nchi kwani wanajua utafuta huu mkataba na kuwabinyia ulaji wao.

Ni vyema ukamwaga manyanga sasa na kustaafu kwani mafao yako hayana mjadala.
 
YUKO WAPI MAKAMU WA RAIS KWENYE HII NGOMA?


Makamu wa Rais ni gwiji wa kutetea haki. Mara nyingi hukemea dhuluma za kijinsia, ukatili dhidi ya wanawake na watoto n.k


Lakini kwenye huu mkataba wa kifisadi kapiga ganzi kulikoni!

Au huchagua mada ambazo hazihatarishi mkate wake kama kutuhubiria maadili mema ya raia wa kawaida.

Wale ambao hawaathiri ajira yake huwa mstari wa mbele kuwashika makoromeo na kuwatishia hatawafumbia macho wakikiuka maadili ya watumishi wa umma.

Sasa tuna zigo la mkataba ambao unatugeuza kuwa watumwa wa waarabu na busara zake zinahitajika lakini tunaona anakwepa kuwakaripia waliotuuza utumwani.

Yaani tumevishwa minyororo na tunakokotwa utumwani na yeye Rais mtarajiwa yaani ni kama hata siyo mkaazi wa nchi hii.

Imekaaje hii?

An inveterate opportunist?


Asichojua 2030, hawa njemba wanajua atachukua fomu ya Urais na jina litakatwa kama la makamu wa Rais waliotangulia.

Majina 5 ya urais ya CCM 2030 ni kwa wale wamo wanautafuna huu mzoga unaitwa DP WORLD kama haumo hawatakuamini kukuachia nchi kwani wanajua utafuta huu mkataba na kuwabinyia ulaji wao.

Ni vyema ukamwaga manyanga sasa na kustaafu kwani mafao yako hayana mjadala.
 
Kauli ya pamoja ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais inaweza kutusaidia baraza la mawaziri likavunjwa mkapoteza tonge lakini mkaingia kwenye historia ya nchi mlikuwa wazalendo wa kweli.

Hutakumbukwa wakati wa shwari bali historia itakukumbuka kwa kujitoa mhanga

Na huo, ndiyo uongozi uliotukuka.

Uongozi siyo wakati wa amani la hasha bali uongozi ni wakati shari.

Hii ni shari siyo shwari na wakati unawadai msimame na kuhesabiwa.

Mpo na haki au mpo na dhuluma.

Hata mkikaa kimya kulinda vitumbua vyenu mjue fika mawe yataongea asema BWANA.
 
JK MWASISI WA HUU MKATABA MBONA KIMYA.


Huu ni mchoro wa JK lakini kakimbilia ubelgiji visingizio kibao huku akiusikilizia muziki kama vile hahusiki.

Lakini haya ni mapigo yake na huyu mama kamwingiza mkenge masikini hata hajui kinachoendelea.

Hajui anatumika tu na hoja yake ya kuwa yeye ni Rais isipokuwa ana jinsia ya kike siyo kweli.

Yeye ni picha na ngoma inachezwa na JK na kikundi chake.

JK rudi utetee huu mkataba wa kitumwa ili wewe na wapambe wako mle kwenye mahangaiko yetu.
 
Kwa wale wote mnaoamini maendeleo ya nchi hii yataletwa na mamluki someni hiki kitabu cha jinsi taifa dogo sana la Israel lilivyowaamini raia yake na kufanya maajabu.


Hivi Israel hawa waarabu tena majirani wake kwani haiwaoni?


Acheni kujidhalilisha na kuikana imani ya KUJITEGEMEA. Tambua tatizo ni nini halafu chukua hatua.


Wote wanaosema matatizo ya bandari zetu ni usimamizi ni waongo.


Matatizo ya bandari zetu ni UWEKEZAJI TU siyo usimamizi.


Hata hao DUBAI PORTS WORLD ukiwaambia wazisimamie bandari zetu bila uwekezaji hakuna la maana watafanya.


Ukitaka kujua uwezo mdogo wa kufikiri wa viongozi wetu ni pale wanauza nchi kwa UWEKEZAJI wa dola za kimarekani milioni 600 tu kwa miaka kumi ijayo.


Hivi hizo TOZO za miamala mnakusanya kiasi gani?

Kwanini hampeleki kuimarisha bandari zetu na kuongeza ufanisi kwa usimamizi wa raia wa nchi hii?




View attachment dan_senor_saul_singer-start-up_nation_the_story_of.pdf
 
Tanzania highest court decision to read and see no evil in blatant violations of our constitution overturned by the Africa Court of Human Rights and peoples Rights....now beyond a shroud of doubt Tanzanian Court of Appeal is too pliant to CCM machinations.


Now we fully understand why Kabudi was hellbent to remove us from the jurisdiction of this Court because it poses an existential threat to election massive rigging of which he and CCM solely depends for his political survival!


PSX_20230613_210818.jpg
 
Mahakama Kuu ya Tanzania ilisema SIO SAWA Wakurugenzi (ma-DED) Kusimamia Uchaguzi.

Mahakama ya Rufani ikatengua Maamuzi hayo[emoji1540], moja ya sababu ilikuwa kwamba Wakurugenzi huwa wanakula kiapo cha kukana vyama vyao vya Siasa, pia hoja ya kwamba wanateuliwa na Rais hivyo hawawezi kukosa upendeleo kwa Chama tawala, Mahakama ikasema hoja hiyo ni ya kubahatisha/dhahania na inatokana na wasiwasi tu, hakuna ushahidi.[emoji848]

Sasa leo Mahakama ya Afrika nayo imetoa neno, imesema SIO SAWA Wakurugenzi Kusimamia Uchaguzi.

Pata wasaa wa kupita nazo, nani yupo sahihi? Mahakama Kuu na Mahakama ya Afrika au Mahakama ya Rufani?[emoji1600]

MD, Mendez (M.C.A)
13/06/2023


MAONI YETU


Mahakama ya Afrika iko sahihi

Mahakama Kuu iko sahihi

Mahakama ya Rufani ziiiiiiii ni tawi la CCM.


Tatizo ni ya kuwa katiba ilivunjwa kwa sababu moja tu sheria za uchaguzi zilikasimu mamlaka ya usimamizi wa chaguzi zetu kwa wakurugenzi wa halmashauri/ majiji kinyume na matakwa ya katiba yanayosema Tume ya uchaguzi ndicho chombo pekee chenye mamlaka ya kusimamia chaguzi zetu

Hoja za mahakama ya rufaa ya kuwa kwa vile DEDs wanaapishwa basi hawapendelei na hakuna ushahidi wanapendelea hazina uhusiano wowote na ukweli kuwa watajwa hao hawajapewa mamlaka ya kikatiba kusimamia chaguzi zetu. Tunashindwa kuelewa hoja za kuwepo upendeleo au kutokuwepo upendeleo zinahusika vipi na katiba kutowatambua wakurugenzi tajwa kusimamia chaguzi zetu?

Hakuna ibara yoyote ya katiba ambayo inairuhusu tume ya uchaguzi kukasimu mamlaka yake ya kikatiba ya kusimamia uchaguzi na hivyo kufanya vifungu vya sheria vinavyoishurutisha Tume kubwaga manyanga kuwa zimekiuka katiba.

Tunachoshindwa kuelewa ni kigugumizi kipi mahakama ya rufaa hupatwa katika kutenda haki.

Ni hizi peremende za vyeo baada ya kustaafu ndiyo mlungula wenyewe au kuna mengine.

Kama ni peremende tajwa basi kuna uhaja wa kuwazuia watumishi wa mahakama kuhongwa na watendaji serikalini kwa maisha yao yote pengine itapunguza makali ya kutoa maamuzi ambayo hayana kichwa wala miguu kama huu.




View attachment MD, Mendez - Bob Chacha Wangwe v. Tanzania , DED to Supervise Election Violates Human Rights, ...pdf



View attachment MD, Mendez - AG v. Bob Chacha Wangwe, DED to Supervise Election is Not Against Constitution, W...pdf





View attachment MD, Mendez - HC Bob Chacha Wangwe, DED to Supervise Election Violates Human Rights, Wakurugenz...pdf
 
Until an inclusive NEC takes charge of our elections, the relationship between voters and their leaders shall remain fatally crooked and debilitating.

There's no such thing called an independent NEC but there's an inclusive NEC.

PRAGMATISM NOT IDEALISM ought to guide this debate. Nobody is free from external influences but what we urgently need is check and balance to constrain and deter those negative duresses when they rear its evil hydra.


Unless we truncate illegal representation, leaders shall continue advocating self interest policies at the detriment of the populace, and ultimately violent redress is the unfortunate comeuppance.


All registered political parties must have a say in the formation of NEC by having representatives or at least a chance of having one.

No political party should have more than 25% composition of commissioners, and the NEC must independently establish and run own secretariat free from political interference.




IMG-20230613-WA0022.jpg
 
Conflicting statements from the same government.

The minister for agriculture said crop harvests belong to peasants and can sell to whomsoever, but his boss has different broadside.

Lack of consistency in government policy confuses investors and many are skeptical in long term vision of this government



As we speak, tons and tons of maize are stranded at Kenyan borders with refusal to issue permits in either side of borders a major hindrance.

At the heart of this hullabaloo, lies peasants in dire need of stable markets and poor urbanites malnourished of real nutrition all that come at a cost pushing poor peasants to subsidize wrecked government policies.

10cab6cb3dcc47d0904c020dcb71c436_352850655_840875560733474_8985324322414226359_n.jpg
 
Presidential appointments brandish 3Rs.

REUSE, REDUCE AND RECYCLE.


Keep wondering Bulembo and Lukuvi notorious failed hands will counsel anything useful.

Anything the duo touches turn into ashes. We thought we hard done by with them but bad habits die hard.

But we are pleased to remind all and sundry that GARBAGE IN GARBAGE OUT.

Slowly but steadily this Presidency is beginning to look like a sick little joke.


IMG-20230613-WA0024.jpg
 



Profesa maji marefu hebu tujibu hili swali ni nani alikuchagua?

Wewe ni tunda la uwakilishi haramu utamhubiria nani?


Swali ambalo hawa mafisadi kamwe hawatajibu ni kwanini Nyerere alienda UN na kuwahakikishia tuko tayari kujitawala?

Kujitawala kunaanzia kwa watanzania kuzisimamia njia kuu za uchumi na wala siyo vinginevyo. Tuendeshe vizuri au la hilo ni jukumu letu.


Matatizo ya Tanzania ni ya kimfumo tu ambayo yamezalisha uwakilishi haramu ambao siyo chaguo la watanzania na matokeo wamekuwa vibaraka wa wakoloni mamboleo.

Hatuna sababu yoyote ile watanzania wasisimamie njia kuu za uchumi.

Watanzania hatujashindwa ila mfumo kandamizi ndiyo umeshindwa kututoa kwenye hili tope tulilokwama.


Majibu mepesi ya kuwamilikisha wakoloni nchi yetu ni viraka tu ambavyo vitaongeza misuguano kwenye jamii na amani itaota mbawa.


Majibu ya kudumu ni kutambua mfumo uliopo umezalisha viongozi ambao ni dhaifu na hawawajibiki kwa wananchi na hivyo hawawezi kuyajali masilahi ya wananchi bali wameweka ulafi wao mbele.

Kutatua haya matatizo ni kuwarudishia wapigakura haki yao ya kuwachagua viongozi ambao wataweka masilahi yao mbele.


Lakini tukiendelea na huu mfumo wa kukasimu madaraka kwa wezi wa kura tutaishia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Amani haiji kwa ulimi tu bali kwa dhamira inayojionyesha kwenye matendo ya kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwatendea haki wanakondoo wake.


Watanzania tu ndiyo wana majibu ya kero zetu siyo wakoloni wawe na uwekezaji hawana, wawe na tekinolojia au hawana siyo sababu ya kuudhalilisha utu wetu.


Wanaosema TUMESHINDWA wajue ni wao wameshindwa kuboresha mfumo wa uwajibikaji ambao ndiyo umetufikisha hapa waache kulaumu wataalamu ambao ni wao wanasiasa uchwara ndiyo huwateua kukidhi masilahi yao binafsi ambayo hata hayawapeleki popote.

Mwisho wa siku wanakufa na huwa tunajiuliza hizi harakati za pimbi huyu kumbe kweli alikuwa zezeta hata hakujua yeye ni keki nono kuliko zote za funza na mang'onyo?
 
Back
Top Bottom