New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Hivi tuna sababu gani ya kutafuta mwekezaji mwingine wakati tayari tunaye.

Hivi kumlipa huyu mwekezaji Tshs 260 Bill inaleta faida kwetu wakati anayekuja hata sumni hatatulipa?

Si kheri huyu ale hata kama hatatulipa kitu kuliko kumjengea mwekezaji mwingine mazingira ya kula lwa gharama yetu huku tukijua hatatuachia kitu zaidi ya mashimo?

Kwa huu uzembe hatuna muda mrefu tutashindwa hata kuwalipa wafanyakazi wa umma mishahara tutabanwa kuwalipa hawa wawekezaji feki
PSX_20230718_191811.jpg
 
Miradi ya Nickel sulphide tuliwapa wawekezaji hawana hela au ujuzi wa kuiendeleza na wao (mining speculators) na wao wakawatafuta wengine waje wawasaidia kula huu mnofu.

Sisi tukawaondoa kwa marekebisho ya sheria ya madini wakati tayari haki wanazo mkononi sasa hawa matapeli wameshinda kesi kwa mikataba ya nchi na nchi

Unamleta mwekezaji hewa naye analeta mwekezaji halisi na anamuuzia 60% ya migodi na yuko tayari kumwuuzia 20% zaidi hata mwekezaji wa awali abakie na 20% ya umiliki hapo inabidi ujiulize tulifikaje huko?


Kwanini STAMICO hawapewi hii migodi wakaichimba?

Kama STAMICO wangelipewa wachimbe hawa wawekezaji feki wasingelikuwepo na hii migogoro pia isingelikuwepo.

IMX Resources inks $60 million joint-venture deal to develop Ntaka Hill Nickel Project


Junior Mining Network | September 25, 2013 | 12:09 am Base Metals China Nickel

IMX Resources inks $60 million joint-venture deal to develop Ntaka Hill Nickel ProjectIMX Resources Ltd. (TSX: IXR) announced this week the company has formed a joint-venture agreement with Hong Kong based MMG Limited (HK: MMG) to advance the Ntaka Hill Nickel Project located in Tanzania.

Terms of the agreement call for MMG to incur $60 million in expenditures over a five year period in exchange for a 60% interest in the Ntaka Hill Project. The agreement also gives MMG the option to acquire an additional 20% interest upon delivery of a Bankable Feasibility Study (BFS) and additional cash payments.

“We are delighted to welcome MMG as our partner to test for deeper, high-grade mafic intrusive style nickel mineralisation at Ntaka Hill and to build on our success to date,” said IMX Managing Director Neil Meadows in the news release. “The deeper exploration program lends itself to a partnership with a large company like MMG to manage the higher cost of such a program, but also to bring to bear additional technical capability.”

The Ntaka Hill Nickel Project contains global National Instrument (NI) 43-101 compliant measured and indicated resources of 20.3 million tonnes grading 0.58% nickel. An additional 35.9 million tonnes grading 0.66% nickel currently reside in the inferred category.

IMX acquired the Nachingwea Regional Project in 2012 as part of its acquisition of Continental Nickel. To date nearly 300 diamond holes spanning over 50,000 meters have been drilled into Ntaka Hill.

IMX released assay results on September 11th from drilling completed over the summer at Ntaka. The drill program, which tested for outlying extensions of the deposit, highlighted 1.2 meters of 1.12% nickel in drill hole NAD13-353 and 21.4 meters of 0.4% nickel in hole NAD13-354.

The joint-venture agreement calls for MMG to immediately become project operator. MMG has plans to shift the exploration focus at Ntaka to test for potential higher-grade mineralization at depth.

Regional exploration will also continue at Nachingwea. IMX has identified over seven kilometers of prospective ultramafic rocks within its land holdings which it believes could host additional massive and disseminated nickel and copper mineralization.

In addition to its Tanzanian holdings, IMX also has a 51% interest in the Cairn Hill Mine located in South Australia. The mine has been in operation since 2010 and has shipped over four million tonnes of high-grade magnetite and copper ore through direct shipping operations.

The company has projected cash flow guidance of $34 million during full year 2013 from Cairn Hill. Additionally, IMX announced in March that the joint-venture would begin testing for copper and gold mineralization at Cairn Hill.

Shares of IMX Resources are traded on the TSX under the ticker symbol IXR and the company also retains an ASX listing under the same symbol. The company has 396 million shares outstanding and holds a market cap of $39.6 million as of Friday’s close.
PSX_20230718_195936.jpg
 
Misri hawatengenezi magari yanayoendeshwa bila dereva sasa huu mwaliko wa makampuni 15 kutoka misri yakusaidie utengeneze magari ya aina hiyo si ni sawasawa na vipofu wawili kuonyeshana njia si watanasa kwenye mtaro?


Misri alishindwa kitu kidogo kama ujenzi wa bwawa la Stigler Gorge hata akawauzia wachina zabuni sasa ataweza kutusaidia tutengeneze magari yanatoenddeshwa bila ya dereva?

Mbaya zaidi siyo kazi ya vyuo kutengeneza magari bali kuwafundisha wanafunzi tu.


Msitutoe kwenye njia kuu.


Tanzania kutengeneza magari, bajaji zisizohitaji dereva
Jumanne, Julai 18, 2023.

By Jesse Mikofu
Mwandishi wa Habari

Mwananchi

Unguja. Katika mkakati wa kukuza Tehama na Ubunifu nchini, Tanzania imealika kampuni 15 za Misri, huku lengo likiwa kuhakikisha katika miaka michache ijayo, Tanzania itengeneze magari na bajaji za umeme na zisizo hitaji dereva


Akizungumza katika maonyesho ya biashara baina ya wafanyabiashara wa Zanzibar na Misri mjini Unguja leo Julai 18, 2023, Mkurugenzi Mkuu Tume ya Teknolojia Habari na Mawasiliano Tanzania (ICTC), Dk Nkundwe Mwasaga amesema Tanzania ina wabunifu wengi.

“Tanzania kuna kampuni ambazo zina ubunifu utakaosaidia kutengeneza magari yanayotumia umeme na tayari kuna watu wameonyesha uwezo huo hivyo kuja kwa kampuni hizo itakuwa fursa ya kuendelza ubunifu huo,” amesama na kuongeza;

“Sasa ili kukuza Tehama na Ubunifu nchini, ICTC imezialika kampuni kubwa 15 za Tehama kutoka nchini Misri kukutana na kampuni za hapa nchini kubadilisha uzoefu na hivyo kuviwezesha vyuo nchini kujenga hayo magari.”

Kwa mujibu wa Dk Nkundwe, magari hayo yatakuwa yanaendeshwa bila kuwa dereva na kwamba mwakampuni hayo yaliyoalikwa wana teknolojia hiyo lakini pia wana ile inayohusu matumizi ya betri ambazo hazitumii umeme mkubwa.

“Na kama uhusiano huu utaendelea vizuri, basi kwa mara ya kwanza Tanzania inaweza kuwa na bajaji na magari yanaendeshwa bila kuwa na dereva, huku yakitumia umeme mdogo, lengo letu ni Tehama nchini,” amesema.


Hivyo Dk Mwasaga amewataka kampuni na watu binafsi wenye ubunifu katika Tehama kuhakikisha wanachangamkia fursa hiyo kupata uzoefu zaidi kukuza Tehama nchini

Naye Meneja Mkuu wa Benki ya Misri, Emad Shawky, amesema ni wakati sasa kati ya kampuni za Tanzania na Misri kushirikiana kukuza biashara na uchumi wa mataifa hayo mawali.

Ofisa kutoka Tantrade ambayo inashirikiana na Fredy Liundi amesema hiyo ni fursa kati ya mataifa hayo mawili kwahiyo watapata uwezo mkubwa kubadilishana uwezo hata kufungua viwanda hapa nchini.


PSX_20230719_102016.jpg
 
Dawa ya deni ni kulilipa tu siyo kujizungusha zungusha kama pia sana sana hapo mnatuongezea zigo la riba ya deni.

Huwezi kutaifisha migodi ya watu bila fidia huo ndiyo ukweli


Summary
The Tanzanian government has been ordered by the International Centre for Settlement of Investment Disputes, a World Bank tribunal, to pay $109.5 million (Sh265 billion) as compensation for breach of obligation to a foreign investor.

Dar es Salaam. The government said yesterday it will appeal against a recent ruling by the International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID), which ordered the country to pay an Australian firm, Indiana Resources Limited (IDA), $109.5 million.
PSX_20230719_175920.jpg
 
UUNDAJI WA KAMATI YA UTEUZI WA TUME YA UCHAGUZI WA KENYA BADO NI KIZUNGUMKUTI


Muundo wa kamati ya uteuzi wa Tume ya uchaguzi wa Kenya baada ya marekebisho ya sheria (2022) haijatua ukakasi wa taasisi ya Rais kutohusika na uteuzi wa wajumbe wa Tume ya uchaguzi.


Sheria ya uteuzi wa kamati ya ajira ya Tume ya uchaguzi imelenga kumwondoa Rais kwenye uteuzi na kuweka kazi ya uteuzi kufanywa na wadau tatizo lengo ni mswano ila utambuzi wa wadau ndiyo mushkeli.

Wajumbe wa kamati ya uteuzi wa Tume ya uchaguzi kutoka kwa warasimu siyo sahihi kwa sababu hawa ni wateule wa Rais kwa namna moja au nyingine na kupoteza lengo la kuiondoa taasisi ya Urais kwenye teuzi ya Tume ya uchaguzi.


Wajumbe wafuatao hawakupaswa kuwa kwenye Tume ya uchaguzi

1) Public Service Commission (1)


2) Parliament Service Commission (2)


3) Political Parties Liason Committee (1)

Ukiangalia hawa ni zaidi ya nusu ya wajumbe wa kamati ya uteuzi yenye wajumbe 7.

Hivyo, hoja za wapinzani ya kuwa hii ni Tume ya Rais zina mashiko ya kutosha kabisa.

Jibu kwenye hili lalamiko ni kuwaondoa hawa wajumbe 4 na nafasi zao kuchukuliwa na makundi mengine:-


1) Chama cha wanasheria wa Kenya waongezewe nafasi 1 na kuwa na nafasi 2 mmoja dume na mwingine jike (2)


2) Wawakilishi wa taasisi za kidini waongezewe kutoka nafasi 2 hadi 4.

Kwa haya marekebisho warasimu serikalini watakuwa hawahusiki katika uteuzi wa Tume ya uchaguzi na kupatia majibu ya malalamiko ya wapinzani juu ya lalamiko wajumbe wa kiserikali wameifunika Kamati ya Uteuzi wa Tume ya uchaguzi.


Wajumbe wote wa kamati ya uteuzi watapatikana kwa chaguzi za wanachama wao na watatumikia kwenye kamati ya uteuzi wa Tume ya vipindi visivyozidi viwili vya miaka 3 kila kipindi.


Tunawakilisha hoja


PSX_20230720_122921.jpg
 



Ruto Appoints Selection Panel For Recruitment Of New IEBC Chair, Commissioners.


However, the selected Panel for the IEBC recruitment is dogged with executive overbearing. 4 of the 7 members of the selection Panel are civil servants, not above executive tweaked.
 
Tumepigwa na kitu kizito kichwani

Wamiliki wa TICTS wamejivua umiliki na kupanda merikebu ya Titanic sasa inaitwa DP WORLD (TANZANIA).


Wengi hili hawalijui wanadhani kwisha habari yao kumbe wamevua umiliki mmoja na kuhamia wa pili na ndiyo maana wanampigia debe la kutosha MWARABU baada ya kumegewa HISA


La ajabu, badala ya kupiga ganzi na kula kimya kimya wanatulaghai kuwa nao pia wamepigwa wakati WAMEULA TENA MLO MKUBWA




IMG-20230720-WA0017.jpg
 
Anaandika Dr.@happy.joseph2 (PhD)
________
Serikali haijui inajibu nini. Hakuna mtu ana tatizo na KAMPUNI ya DP World. Watanzania wana tatizo na kilichoandikwa kwenye mkataba. Hata kama mkataba ungetolewa kwa kampuni NYINGINE YOYOTE (iwe ya Marekani, China, Ulaya), kwa aina ile ya mkataba, bado tungelalamika.

Watanzania wanaongelea mambo haya;

1. Suala la MUDA wa mkataba.

2. Kampuni ya kigeni kumilikishwa ardhi.

3. Mkataba kutokuweza kuvunjwa kwa namna yeyote ile.

4. Serikali kukosa uwezo wa kukagua kinachofanyika bandarini.

5. Uendeshwaji wa BANDARI ZOTE (Tunataka wapewe BAADHI ya bandari) au DP world ifanye ubia na serikali (PPP) sio kubeba bandari zote kama mali yao.

6. Serikali kutokuruhusiwa kutazama fursa nyingine mpaka DP world waulizwe kwanza (yaani hata kama hawawezi wakikataa serikali inakosa nguvu).

7. Hakuna tangible results (matokeo/manufaa halisi) toka kwa DP world. Mkataba unasema kwa ujumla tu kwamba mafanikio yatakuwepo ila hayasemwi ni yapi na kwa kiasi gani.

Maelezo ya Waziri Mbarawa kwamba DP World imechaguliwa kwenye mchakato wa kampuni 7 hayana maana. Sisi hatuna shida na mchakato wa kuchagua kampuni za kuwekeza. Tuna shida na makubaliano yaliyoafikiwa.

Serikali kutumia nguvu kubwa kuelezea mambo YASIYOHUSIANA na hoja za wananchi ni ishara kuwa HAWANA MAJIBU ya maswali tunayouliza, na hivyo wameamua kuongea-ongea tu ili waonekane na wao hawajakaa kimya.

Tunachokitaka kutoka kwa serikali si KUZUNGUMZA kile wanachokitaka, bali ni KUTOA MAJIBU ya kile sisi wananchi tunachotaka. Yani wajibu maswali na hoja zetu sio kuibua vitu vingine nje ya hoja za wananchi.

Kuliko viongozi wa serikali kuongea vitu visivyojibu hoja za wananchi, bora waseme kama mambo yameshaharibika tujue moja. Watuambie kwamba walishajifunga kitanzi na hivyo kujibu au kutokujibu hakubadilishi kitu kwenye mkataba. Itatusaidia tujue namna nyingine ya kushughulikia suala hili, maana kwa sasa ni kama vile tunaongea na viziwi.

Yani kila kiongozi akisimama anaeleza vitu vyake. Na hivyo anavyoeleza havijibu hata kidogo hoja za wananchi. Wanaongea tu ili mradi waonekane hawajakaa kimya. Hi si sawa hata kidogo.

Wasalaam,
Happy Wa Joseph (BIBI).!
 
Kesho tutalipitia upya wazo letu la ni jinsi gani watanganyika watakuwa na sauti katika mambo yasiyo ya Muungano ili nyakati zote watanganyika wawe ma wawakilishi wao katika usimamizi wa maliasili zao kama ilivyo kwa Zanzibar

Zanzibar ni nchi kwenye mambo yasiyo ya Muungano hivyo ni sahihi kwa Tanganyika kuwa nchi kwenye mambo yasiyo ya Muungano vinginevyo hizi dosari zinaweza kuishia kuuvunja Muungano.


Wengi wape usipowapa watajinyakulia. Pia mambo ya Muungano yapunguzwe na kubaki machache hususani ulinzi na usalama, mambo ya kigeni tu.


Elimu, mawasiliano, fedha, madini n.k yasimamiwe na kila nchi.

Zanzibar wawe na uwakilishi wa mashirika ya kimataifa kama UN, EAC, AU n.k na idadi ya mabalozi kama watakavyohitaji ila kwa gharama zao.
 
Back
Top Bottom