Anaandika
Dr.@happy.joseph2 (PhD)
________
Serikali haijui inajibu nini. Hakuna mtu ana tatizo na KAMPUNI ya DP World. Watanzania wana tatizo na kilichoandikwa kwenye mkataba. Hata kama mkataba ungetolewa kwa kampuni NYINGINE YOYOTE (iwe ya Marekani, China, Ulaya), kwa aina ile ya mkataba, bado tungelalamika.
Watanzania wanaongelea mambo haya;
1. Suala la MUDA wa mkataba.
2. Kampuni ya kigeni kumilikishwa ardhi.
3. Mkataba kutokuweza kuvunjwa kwa namna yeyote ile.
4. Serikali kukosa uwezo wa kukagua kinachofanyika bandarini.
5. Uendeshwaji wa BANDARI ZOTE (Tunataka wapewe BAADHI ya bandari) au DP world ifanye ubia na serikali (PPP) sio kubeba bandari zote kama mali yao.
6. Serikali kutokuruhusiwa kutazama fursa nyingine mpaka DP world waulizwe kwanza (yaani hata kama hawawezi wakikataa serikali inakosa nguvu).
7. Hakuna tangible results (matokeo/manufaa halisi) toka kwa DP world. Mkataba unasema kwa ujumla tu kwamba mafanikio yatakuwepo ila hayasemwi ni yapi na kwa kiasi gani.
Maelezo ya Waziri Mbarawa kwamba DP World imechaguliwa kwenye mchakato wa kampuni 7 hayana maana. Sisi hatuna shida na mchakato wa kuchagua kampuni za kuwekeza. Tuna shida na makubaliano yaliyoafikiwa.
Serikali kutumia nguvu kubwa kuelezea mambo YASIYOHUSIANA na hoja za wananchi ni ishara kuwa HAWANA MAJIBU ya maswali tunayouliza, na hivyo wameamua kuongea-ongea tu ili waonekane na wao hawajakaa kimya.
Tunachokitaka kutoka kwa serikali si KUZUNGUMZA kile wanachokitaka, bali ni KUTOA MAJIBU ya kile sisi wananchi tunachotaka. Yani wajibu maswali na hoja zetu sio kuibua vitu vingine nje ya hoja za wananchi.
Kuliko viongozi wa serikali kuongea vitu visivyojibu hoja za wananchi, bora waseme kama mambo yameshaharibika tujue moja. Watuambie kwamba walishajifunga kitanzi na hivyo kujibu au kutokujibu hakubadilishi kitu kwenye mkataba. Itatusaidia tujue namna nyingine ya kushughulikia suala hili, maana kwa sasa ni kama vile tunaongea na viziwi.
Yani kila kiongozi akisimama anaeleza vitu vyake. Na hivyo anavyoeleza havijibu hata kidogo hoja za wananchi. Wanaongea tu ili mradi waonekane hawajakaa kimya. Hi si sawa hata kidogo.
Wasalaam,
Happy Wa Joseph (BIBI).!