New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Hivi tuna sababu gani ya kutafuta mwekezaji mwingine wakati tayari tunaye.

Hivi kumlipa huyu mwekezaji Tshs 260 Bill inaleta faida kwetu wakati anayekuja hata sumni hatatulipa?

Si kheri huyu ale hata kama hatatulipa kitu kuliko kumjengea mwekezaji mwingine mazingira ya kula lwa gharama yetu huku tukijua hatatuachia kitu zaidi ya mashimo?

Kwa huu uzembe hatuna muda mrefu tutashindwa hata kuwalipa wafanyakazi wa umma mishahara tutabanwa kuwalipa hawa wawekezaji feki
 
Miradi ya Nickel sulphide tuliwapa wawekezaji hawana hela au ujuzi wa kuiendeleza na wao (mining speculators) na wao wakawatafuta wengine waje wawasaidia kula huu mnofu.

Sisi tukawaondoa kwa marekebisho ya sheria ya madini wakati tayari haki wanazo mkononi sasa hawa matapeli wameshinda kesi kwa mikataba ya nchi na nchi

Unamleta mwekezaji hewa naye analeta mwekezaji halisi na anamuuzia 60% ya migodi na yuko tayari kumwuuzia 20% zaidi hata mwekezaji wa awali abakie na 20% ya umiliki hapo inabidi ujiulize tulifikaje huko?


Kwanini STAMICO hawapewi hii migodi wakaichimba?

Kama STAMICO wangelipewa wachimbe hawa wawekezaji feki wasingelikuwepo na hii migogoro pia isingelikuwepo.

 
Misri hawatengenezi magari yanayoendeshwa bila dereva sasa huu mwaliko wa makampuni 15 kutoka misri yakusaidie utengeneze magari ya aina hiyo si ni sawasawa na vipofu wawili kuonyeshana njia si watanasa kwenye mtaro?


Misri alishindwa kitu kidogo kama ujenzi wa bwawa la Stigler Gorge hata akawauzia wachina zabuni sasa ataweza kutusaidia tutengeneze magari yanatoenddeshwa bila ya dereva?

Mbaya zaidi siyo kazi ya vyuo kutengeneza magari bali kuwafundisha wanafunzi tu.


Msitutoe kwenye njia kuu.




 
Dawa ya deni ni kulilipa tu siyo kujizungusha zungusha kama pia sana sana hapo mnatuongezea zigo la riba ya deni.

Huwezi kutaifisha migodi ya watu bila fidia huo ndiyo ukweli


 
UUNDAJI WA KAMATI YA UTEUZI WA TUME YA UCHAGUZI WA KENYA BADO NI KIZUNGUMKUTI


Muundo wa kamati ya uteuzi wa Tume ya uchaguzi wa Kenya baada ya marekebisho ya sheria (2022) haijatua ukakasi wa taasisi ya Rais kutohusika na uteuzi wa wajumbe wa Tume ya uchaguzi.


Sheria ya uteuzi wa kamati ya ajira ya Tume ya uchaguzi imelenga kumwondoa Rais kwenye uteuzi na kuweka kazi ya uteuzi kufanywa na wadau tatizo lengo ni mswano ila utambuzi wa wadau ndiyo mushkeli.

Wajumbe wa kamati ya uteuzi wa Tume ya uchaguzi kutoka kwa warasimu siyo sahihi kwa sababu hawa ni wateule wa Rais kwa namna moja au nyingine na kupoteza lengo la kuiondoa taasisi ya Urais kwenye teuzi ya Tume ya uchaguzi.


Wajumbe wafuatao hawakupaswa kuwa kwenye Tume ya uchaguzi

1) Public Service Commission (1)


2) Parliament Service Commission (2)


3) Political Parties Liason Committee (1)

Ukiangalia hawa ni zaidi ya nusu ya wajumbe wa kamati ya uteuzi yenye wajumbe 7.

Hivyo, hoja za wapinzani ya kuwa hii ni Tume ya Rais zina mashiko ya kutosha kabisa.

Jibu kwenye hili lalamiko ni kuwaondoa hawa wajumbe 4 na nafasi zao kuchukuliwa na makundi mengine:-


1) Chama cha wanasheria wa Kenya waongezewe nafasi 1 na kuwa na nafasi 2 mmoja dume na mwingine jike (2)


2) Wawakilishi wa taasisi za kidini waongezewe kutoka nafasi 2 hadi 4.

Kwa haya marekebisho warasimu serikalini watakuwa hawahusiki katika uteuzi wa Tume ya uchaguzi na kupatia majibu ya malalamiko ya wapinzani juu ya lalamiko wajumbe wa kiserikali wameifunika Kamati ya Uteuzi wa Tume ya uchaguzi.


Wajumbe wote wa kamati ya uteuzi watapatikana kwa chaguzi za wanachama wao na watatumikia kwenye kamati ya uteuzi wa Tume ya vipindi visivyozidi viwili vya miaka 3 kila kipindi.


Tunawakilisha hoja


 


Ruto Appoints Selection Panel For Recruitment Of New IEBC Chair, Commissioners.


However, the selected Panel for the IEBC recruitment is dogged with executive overbearing. 4 of the 7 members of the selection Panel are civil servants, not above executive tweaked.
 
Tumepigwa na kitu kizito kichwani

Wamiliki wa TICTS wamejivua umiliki na kupanda merikebu ya Titanic sasa inaitwa DP WORLD (TANZANIA).


Wengi hili hawalijui wanadhani kwisha habari yao kumbe wamevua umiliki mmoja na kuhamia wa pili na ndiyo maana wanampigia debe la kutosha MWARABU baada ya kumegewa HISA


La ajabu, badala ya kupiga ganzi na kula kimya kimya wanatulaghai kuwa nao pia wamepigwa wakati WAMEULA TENA MLO MKUBWA




 
Anaandika Dr.@happy.joseph2 (PhD)
________
Serikali haijui inajibu nini. Hakuna mtu ana tatizo na KAMPUNI ya DP World. Watanzania wana tatizo na kilichoandikwa kwenye mkataba. Hata kama mkataba ungetolewa kwa kampuni NYINGINE YOYOTE (iwe ya Marekani, China, Ulaya), kwa aina ile ya mkataba, bado tungelalamika.

Watanzania wanaongelea mambo haya;

1. Suala la MUDA wa mkataba.

2. Kampuni ya kigeni kumilikishwa ardhi.

3. Mkataba kutokuweza kuvunjwa kwa namna yeyote ile.

4. Serikali kukosa uwezo wa kukagua kinachofanyika bandarini.

5. Uendeshwaji wa BANDARI ZOTE (Tunataka wapewe BAADHI ya bandari) au DP world ifanye ubia na serikali (PPP) sio kubeba bandari zote kama mali yao.

6. Serikali kutokuruhusiwa kutazama fursa nyingine mpaka DP world waulizwe kwanza (yaani hata kama hawawezi wakikataa serikali inakosa nguvu).

7. Hakuna tangible results (matokeo/manufaa halisi) toka kwa DP world. Mkataba unasema kwa ujumla tu kwamba mafanikio yatakuwepo ila hayasemwi ni yapi na kwa kiasi gani.

Maelezo ya Waziri Mbarawa kwamba DP World imechaguliwa kwenye mchakato wa kampuni 7 hayana maana. Sisi hatuna shida na mchakato wa kuchagua kampuni za kuwekeza. Tuna shida na makubaliano yaliyoafikiwa.

Serikali kutumia nguvu kubwa kuelezea mambo YASIYOHUSIANA na hoja za wananchi ni ishara kuwa HAWANA MAJIBU ya maswali tunayouliza, na hivyo wameamua kuongea-ongea tu ili waonekane na wao hawajakaa kimya.

Tunachokitaka kutoka kwa serikali si KUZUNGUMZA kile wanachokitaka, bali ni KUTOA MAJIBU ya kile sisi wananchi tunachotaka. Yani wajibu maswali na hoja zetu sio kuibua vitu vingine nje ya hoja za wananchi.

Kuliko viongozi wa serikali kuongea vitu visivyojibu hoja za wananchi, bora waseme kama mambo yameshaharibika tujue moja. Watuambie kwamba walishajifunga kitanzi na hivyo kujibu au kutokujibu hakubadilishi kitu kwenye mkataba. Itatusaidia tujue namna nyingine ya kushughulikia suala hili, maana kwa sasa ni kama vile tunaongea na viziwi.

Yani kila kiongozi akisimama anaeleza vitu vyake. Na hivyo anavyoeleza havijibu hata kidogo hoja za wananchi. Wanaongea tu ili mradi waonekane hawajakaa kimya. Hi si sawa hata kidogo.

Wasalaam,
Happy Wa Joseph (BIBI).!
 
Kesho tutalipitia upya wazo letu la ni jinsi gani watanganyika watakuwa na sauti katika mambo yasiyo ya Muungano ili nyakati zote watanganyika wawe ma wawakilishi wao katika usimamizi wa maliasili zao kama ilivyo kwa Zanzibar

Zanzibar ni nchi kwenye mambo yasiyo ya Muungano hivyo ni sahihi kwa Tanganyika kuwa nchi kwenye mambo yasiyo ya Muungano vinginevyo hizi dosari zinaweza kuishia kuuvunja Muungano.


Wengi wape usipowapa watajinyakulia. Pia mambo ya Muungano yapunguzwe na kubaki machache hususani ulinzi na usalama, mambo ya kigeni tu.


Elimu, mawasiliano, fedha, madini n.k yasimamiwe na kila nchi.

Zanzibar wawe na uwakilishi wa mashirika ya kimataifa kama UN, EAC, AU n.k na idadi ya mabalozi kama watakavyohitaji ila kwa gharama zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…