View: https://youtu.be/WIO8uBaEibc
Kubadilisha sheria ili kumnufaisha mwekezaji mmoja tu ni kumpendelea na kwa kufanya hivyo ni kukiuka katiba kwa kuondoa usawa kwa wote
Si bunge au mahakama inaheshimu ukatiba kwenye hili sakata kwa kuwa huu sasa ni mlo wa wanasiasa wa kitaifa.
Hata ukiwapa maoni yako bunge watayatupilia mbali maana hawako kukutumikia wewe bali kuyatumikia matumbo yao.
Na kukaribisha maoni ya wananchi wakati tayari wana azimio lao la kibunge kiganjani ni uthibitisho wa uwazi wa unafiki wao.
Hata ukienda mahakamani wataikana katiba ili mradi wezi wa mali ya umma waendelee kula.
Hii ndiyo Tanzania ambayo tunajaribu kuijenga ambayo viongozi wa kitaifa wapo madarakani siyo kwa masilahi ya wengi bali ya kwao na wawapendao.
Sisi wengine ni kulishwa maneno matamu matamu tu ya kutupa matumaini hewa.
Lakini hii sasa ni laana yao ya ulafi. Watakula na kuvimbiwa lakini hawatashiba. Kila mlo watateswa na uroho wao. Watalala vitandani lakini hawatapata usingizi kwa sababu watateswa na ulafi wao.
Watalindwa na askari lakini mioyoni mwao watakosa amani na maisha yao yote watagubikwa na khofu ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.
Uzao wao utabughia madawa ya kulevya na watazama kwenye ngono hadi magonjwa yasiyosikia tiba kuwatoa uhai wao.
Mafisadi watakesha misibani na mahospitalini wakishindiliwa madawa na hata kwenye sherehe watajisikia wana majonzi na wanaumwa kwa sababu wamemkana Mwenyezi Mungu ambaye angeliwafariji kama wangeliikana hii dunia na mambo yake yote.
Watajiita ni matajiri kumbe ni masikini wa kutupwa na wapweke.