“TANESCO yatumia Sh75 bilioni kukodi software kwa miezi 30”
Ndg January Makamba umetumia (Sh75 bilioni) kukodi ERP software, wakati kuna vitongoji 37,610 kati ya 64,760 havijapata umeme? Nchi isiyo na umeme wa kutosha tunazo 1,605MW tu unatumia US$30M kukodi Enterprise Resources Planning (ERP) software kwa Tech Mahindra? eGA kazi yake? Matusi!
Lengo la TANESCO kusaini mkataba huo wa Sh75 bilioni (US$30 million) na kampuni kutoka India, Tech Mahindra wametueleza kwamba ni kusaidia kuboresha utoaji huduma kwa mtandao. Wakati huo serikali ina huduma yake inaitwa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Enterprise Resources Planning (ERP) ni mfumo wa mipango wa rasilimali za biashara kazi yake ni kutambua kwa haraka masuala yanayowaathiri wateja na wafanyakazi na kuyatatua kwa haraka. Kazi ambayo inafanywa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) tayari walishatengeneza mfumo kama huo na unatumiwa na Taasisi mbali mbali za Serikali, unaitwa Enterprise Resources Management Suite (ERMS). Huu mfumo mwingine wa January Makamba na wahindi wa Tech Mahindra una kipi cha ziada?
Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) ambao ndiyo wenye jukumu la kusimamia pia Enterprise Resources Management Suite (ERMS) ipo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Rais analifahamu jambo hili, na kama hafahamu wanamficha.
Wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS). Software ya aina hii inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Kwa kuwa TANESCO wamekodi, waendeshaji ni wahindi.
Kumbuka, hizi Sh75 bilioni ni fedha ambazo zimetumika kukodi Enterprise Resources Planning (ERP) software kutoka Tech Mahindra kwa miezi 30 tu. Kwamba wahindi wamekodisha (siyo kuuza) mifumo kwa miezi 30 kwa faida ya Sh75 bilioni.
Ukiingia katika tovuti za selecthub na betterbuys, wamekupa gharama (cost) ya ERP and budget guide. Bei ya juu ya kununua Enterprise Resources Planning (ERP) software ni US$10 million (Sh25 bilioni). Kununua siyo kukodi. TANESCO wamekodi kwa US$30 million (Sh75 bilioni)
Zabuni hii ilitangazwa nyakati za mwisho za utawala wa Jakaya Kikwete, haikufanikiwa. Alipoingia Rais John Magufuli akasitisha mpango huo. Alipoingia Rais Samia Suluhu Hassan na kumteua January Makamba kuwa waziri wa Nishati, mpango umefufuliwa na nchi imekodi software.
Kama Enterprise Resources Management Suite (ERMS) ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) haijaunganishwa (integratable) na mifumo mingine ya taasisi za serikali hadi tutumie Sh75 bilioni kukodi software kwa miezi 30 ni wazi nchi yetu hatuna programmers. Nchi mfu.
Lakini, ukisoma specifications za Enterprise Resources Management Suite (ERMS) ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) inaeleza wazi kuwa ni shirikishi (interoperable) na mifumo mingine ya taasisi za serikali. Ghafla tu tuelezwe mifumo haisomani tena? Hapana.
Hatuwezi kuendesha kila kitu wenyewe, tunakodi wataalam kuendesha hadi mifumo ya shirika la umeme? Wakati fulani TANESCO ilibinafsishwa kwa makaburu wa Afrika Kusini kwa hoja kwamba shirika limeshindwa kujiendesha hivyo wapewe wageni, nchi ikaingia gizani ikazaliwa RICHMOND na IPTL.
PS; Software kama hizi kwanini serikali isiwezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini (GePG) ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.
University of Dar es Salaam - College of Engineering and Technology (CoET) wanafundishwa nini kama Shirika la umeme (TANESCO) linaweza kwenda kutumia Sh75 bilioni kwa miezi 30 tu kukodi Enterprise Resources Planning (ERP) software kwa Tech Mahindra?
Ushauri; Kukodi ni mbinu mpya ya software developers ili uwe mteja wao wa milele. Kuna software nyingi unanunua mara 1 na unapata free lifetime upgrades and updates. Ukikodi, mfumo ukisumbua kidogo wataalaam wanakuja unawalipia kila kitu ikiwepo perdiem kwa rate za dollars. Akili.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila