Wanaosema Nyerere na Mwinyi waliwateua Dr. Salim Ahmed Salim na Augustine Mrema kuwa Manaibu waziri wakuu tungependa kuwakumbusha katiba za wakati ule siyo hii ya sasa ambayo uwaziri mkuu huthibitishwa na bunge kwa mteule kupata zaidi ya nusu ya kura za wabunge wote na majukumu yake yameainishwa kiustadi zaidi
Mamlaka ya uwaziri mkuu ni ya kikatiba na yamewekwa bayana ikiwemo kuhusishwa katika uteuzi wa mawaziri, kusimamia na kuratibu shughuli za serikali.
Kama aliyepo anaonekana anapwaya ni kumwondoa na kuteua mwingine ila siyo hii hamirojo hailiki.
Rais hana mamlaka ya kumpunguzia waziri mkuu mamlaka yake ya kikatiba kama ilivyofanyika hapa.
Busara zitumike na kutengua uteuzi batili wa naibu waziri mkuu ni nafasi haiko kikatiba.
Tuna kero nyingi za ukatiba haramu msiendelee kuchochea marumbano ambayo hayana tija.
Sana sana ni mikwaruzano tu na migongano mnaibua kati ya nafasi za kikatiba na zisizo za kikatiba