Wanayoyapenda ni mlo wao kama mafao ya wenza wao na sasa wameongeza chumvi hata familia zao ambayo haimo kwenye Rasimu tajwa zilipwe 60% ya mshahara wa sasa wa Rais aliyeko madarakani endapo kiongozi wa kitaifa ameaga dunia.
Hawatakiwi kusaka tonge kama wengine wao ni kula tu bila ya kufanya kazi.
Kwetu huwa tunakumbushwa mara kwa mara maandiko yasemavyo:-
Wasiyoyapenda hawayafanyii kazi kwa visingizio wananchi hawaijui katiba kwa hiyo wapewe darasa kwanza kabla ya kuanza mchakato wa marekebisho ya katiba
Kwenye hili darasa wamejipa miaka 3 ili wavuke salama uchaguzi wa 2024 na 2025 bila makovu au vidonda-ndugu maana wateule wao wanaoitwa wakurugenzi wa majiji na Halmashauri (makada wa CCM) wapo kumalizana na wapigakura.
Ni wizi wa kura kwenda mbele 😃 😀 😄 😁 🤣 😂 😃 😀 😄 😁 🤣
Kwa hiyo, wanatunga sheria za kawaida za mafao za wenza wao na familia zao kuwa ni ofisi za umma ili walipwe donge nono bila umakini ofisi hizo za umma ni za kikatiba haziwezi kuboreshwa au kutenguliwa na sheria za kawaida.
Mahakama hazitajibu hoja za kisheria za wenza na familia za viongozi wa kitaifa ni ofisi za umma hadi walipwe mafao kulingana na sheria za utumishi wa umma?
Walengwa hawa ni waajiriwa wa umma na kwanini hawalipwi mishahara lakini mafao yanawahusu?