New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Kuna mambo au ibara kwenye rasimu ya warioba ya katiba ambayo serikali inayapenda na yako ambayo haiyapendi
 
Wanayoyapenda ni mlo wao kama mafao ya wenza wao na sasa wameongeza chumvi hata familia zao ambayo haimo kwenye Rasimu tajwa zilipwe 60% ya mshahara wa sasa wa Rais aliyeko madarakani endapo kiongozi wa kitaifa ameaga dunia.

Hawatakiwi kusaka tonge kama wengine wao ni kula tu bila ya kufanya kazi.

Kwetu huwa tunakumbushwa mara kwa mara maandiko yasemavyo:-

"...na asiyefanya kazi na asile."

Hii amri ya Mwenyezi Mungu haiwahusu hata chembe!
 
Wasiyoyapenda hawayafanyii kazi kwa visingizio wananchi hawaijui katiba kwa hiyo wapewe darasa kwanza kabla ya kuanza mchakato wa marekebisho ya katiba
 
Kwenye hili darasa wamejipa miaka 3 ili wavuke salama uchaguzi wa 2024 na 2025 bila makovu au vidonda-ndugu maana wateule wao wanaoitwa wakurugenzi wa majiji na Halmashauri (makada wa CCM) wapo kumalizana na wapigakura.

Ni wizi wa kura kwenda mbele 😃 😀 😄 😁 🤣 😂 😃 😀 😄 😁 🤣
 
Ikija masilahi yao ambayo yamo kwenye rasimu ya warioba hayo hayacheleweshwi kusubiri mchakato wa marekebisho ya katiba
 
Kwa hiyo, wanatunga sheria za kawaida za mafao za wenza wao na familia zao kuwa ni ofisi za umma ili walipwe donge nono bila umakini ofisi hizo za umma ni za kikatiba haziwezi kuboreshwa au kutenguliwa na sheria za kawaida.
 
Wanajua vizuri ila mahakama kwa kuwa wameziweka mfukoni wanajiona wako salama salimini
 
Mahakama zitakejeli hoja zote za ukiukwaji wa katiba na kwenda mbali ya hapo kwa kuhoji uelewa wa sheria wa walalamikaji
 
Mahakama zitajigamba bunge halijatumia mwanya wa kutunga sheria za kawaida kurekebisha katiba
 
Bali bunge limetenda wajibu wake wa kikatiba wa kutunga sheria na katiba hajakiukwa
 
Mahakama hazitajibu hoja za kisheria za wenza na familia za viongozi wa kitaifa ni ofisi za umma hadi walipwe mafao kulingana na sheria za utumishi wa umma?

Walengwa hawa ni waajiriwa wa umma na kwanini hawalipwi mishahara lakini mafao yanawahusu?
 
Hiyo khoja ya kisheria watapiga ganzi kama vile haipo mbele yao. Hivi ndivyo mahakama zetu zinavyolinda viwavi jeshi serikalini
 
Mahakama zetu haziwezi kujibu hoja tajwa kwa sababu wataibua swali jingine
 
Hawa wenza na familia za mstaafu ni watumishi wa umma kulingana na sheria ya utumishi wa umma?
 
Back
Top Bottom