Hata kwa bunge hili hili haijalishi. Pia CCM hawawezi wakakubali uchaguzi urudiwe au kesi zifunguliwe kirahisi. Kikwete in kweli alituuza kwenye swala la katiba.
Lakini kwa sasa cha muhimu ni kuweka mkazo(pressure) ya kutosha. Na hii inahitaji kujitoa kweli kweli.
Vyama vya upinzani vinahitaji kutoshiriki uchaguzi wowote hadi katiba mpya inayoeleweka ipatikane.
Shida wanajisahau. Wao wakipata ubunge/udiwani wanaridhika na kuacha kusisitiza swala la katiba. Wanasahau huwa wanapita kwa "hisani" tu. Akitokea mtu kama Magufuli ambae hajali, wanapokonywa viti vyao kinguvu na hamna kitu wanaweza kufanya, kama ilivyotokea 2020. Wanaishia kung'ung'unika. Kwasababu kiuhalisia katiba iliyopo haiwapi nguvu kudai na kupata haki zao.
Vyama vya wafanyakazi pia inabidi vi-coordinate migomo katika kila sector.
Wanafunzi pia wagome/waandamane.
Mfano tu afrika kusini(Soweto), china(Tienanmen square) na juzi kati hong Kong, maandamano ya wanafunzi yamewasumbua na kuwaumiza vichwa watawala. Tanzania tu migomo ya wanafunzi inawatiaga kiwewe, hadi saa zingine vyonbo vya dola vinaingilia kati.
Vyote hivi vifanyike huku makundi hayo yakisisitiza katiba mpya. Halafu uone kama CCM hawajaanza wenyewe kutafuta watu kwaajili ya maridhiano ili mchakato wa katiba mpya uanze.
Shida ni huwa tunadanganyika na maneno matamu + uoga + kutokujitoa, ndo maana kila leo tunaishia kuongea vitu vile vile, ila hamna kinachobadilika. Kwasababu CCM hawapati pressure yoyote kutoka kwa wananchi, na kuendelea kuhisi kuwa wanatumudu. We need to prove them wrong.
Honestly Askofu Mwamakula alikuwa on to something kuhusu maandamano ya kudai katiba sema alikosa support ya kutosha.